Sunday, June 1, 2008

Mishikaki ya nyama ya ngombe

NYAMA ni miongoni mwa vyakula vilivyo na mapishi ya aina nyingi, ambapo mara kwa mara imekuwa ikibadilika majina kutokana na aina ya upishi au namna ilivyo changanywa katika upishi husika.

ifuatayo namna ya kutengeneza mishikaki ya nyamna ya ngombe ikiwa ni moja kati ya aina lukuki za mapishi ya nyama.

Kabla ya kutengeneza mishikaki kwanza kabisa inbakubidi uelewe aina ya nyama ambayo hutumika kutengenezea mishikaki hiyo ili usije jichanganya katika mapsihi yako.

Nyama aina ya “fillet” ndio hasa inayotakiwa katika upishi huu ingawaje wapishi wengi wamekuwa wakitumia nyama yeyote isiyo na mfupa katika kukamilsisha upishi huu.

Mahitaji

Nyama ya ngombe ( filet) 1/2 kilo
Tangawizi iliyotwangwa vijiko 3 vya chakula
Kitunguu saumu kijiko 1 kikubwa cha chakula
Ndimu 1
Chumvi kijiko 1 cha mezani
Masala kiasi (kama utapendelea)
Karoti kiasi
Hoho kiasi
Kitunguu maji kiasi.

Namna ya kutengeneza

Chukua nyama isafishe vizuri kwa maji safi kisha ikatekate vipande vidogovidogo
weka katika sufuria na kisha kamulia ndimu kipande, weka chumvi kiasi, tangawizi na vitunguu saumu vilivyosagwa,
Chukua hoho karoti na vitunguu maji vikatekate kulingana na vipande vya nyama ulivyokata.
Loweka kwa muda wa dakika 15 kisha chomeka katika miti ya kuchomea ukichanganya na viapande vya hoho na karoti bila kusahau vitunguu maji, kisha Andaa jiko la kuchomea na anza kuchoma.
Hakikisha mishikaki imeiva vizuri bila kuungua kwa matokeo mazuri waweza kuichovya kwenye mafuta kidogo ili kuifanya iive haraka.

Baada ya ya dakika 20 mishikaki yako itakuwa tayari kwa kuliwa, waweza kula na chips au hata ugali.

Kababu za mayaiKABABU ni kitafunwa kilichobuniwa kitaalamu zaidi na kukifanya kuonekana cha kuvutia kutokana na umbo na hata ladha yake?

Lakini pamoja na uzuri wake ni watu wachache sana wanafahamu namna ya kutengeneza upishi huu.
Nimeamua kukuletea upishi huu kutokana na maombi ya watu wengi kutaka maelezo ya namna ya kupika kitafunwa hiki.

Fuatana nami upate uhondo huu

mahitaji


Nyama ya kusaga 1/2kg
Mayai 9
kitunguu saumu kiasi
Vitunguu maji kiasi saga
Tangawizi(mbichi) saga
Chumvi kiasi
pilipili manga kiasi
mafuta ya kula lita moja
Mikate wa boflo1
na pilipili kali kiasi kama unatumia.

Namna ya kutengeneza


1) Chukua tangawizi ,kitunguu maji , kitunguu saumu twanga hadi vilainike kisha weka pembeni.
Halafu chukua nyama yako weka chimvi kisha injika jikoni hadi iive halafu ipua.
Chukua mkate wako toa ile nyama ya ndani na kisha uloweke hadi uloanekisha kamua halafu changanya na nyama pamoja na viungo ulivyotwanga kisha weka unga wa pilipili manga huku ukiendelea kuchaganya, ukichanganyika vizuri weka pembeni.
Chukua mayai sita kati ya tisa yachemshe na kisha yamenye halafu weka pembeni.

Chukua mayai matatu yapasue kisha weka chumvi kidogo halafu weka katika bakuli yake.
Tengeneza maduara sita ya kiasi kisha ya huo mchanganyiko kisha weka yai katika kila duara.
Halafu injika jikoni mafuta yakipata moto chovya maduara yako na kisha weka jikoni hadi yawe ya kahawia.Kababu zako

Supu ya uyoga

SUPU ya uyoga ni maarufu sana na inapendwa na watu wengi. Na mara nyingi upikaji wake unatofautiana na kulingana na matakwa ya walaji.

Katika mapishi leo hii nitakuletea namna ya kupika supu ya uyoga na maziwa upishi ambao ni adimu sana kwa walaji walio wengi.

Mahitaji

Uyoga ¼
Unga wa ngano kijiko cha chakula
Margarine (blue band) kijiko cha chakula
Maziwa kikombe kimoja cha chai
Kitunguu saumu viwili vikubwa
Tangawizi mbili kubwa
Chumvi. kiasi

Namna ya kupika

Chukua uyoga wako usafishe na kisha katakata vipande vidogovidogo, halafu kitunguu maji katakata weka kwenye sufuria,chukua tangawizi na kitunguu saumu twanga changanya pamoja, weka chumvi halafu tia lita mbili za maji katika sufuria hilo na kisha chemsha kwa muda wa dakika 20.
Acha ichemke hadi ibakie ujazo wa lita moja au moja na nusu.
Pasha margarine au siagi kaaanga unga wa ngano mkavu hadi ubadilike rangi na kuwa brown, weka maziwa huku ukikoroga.
Endelea kukoroga kwa muda wa dakika 2 hadi 3 kisha weka mchanganyiko uliochemsha awali na endelea kukorga hadi vichanganyike vizuri.
Acha vichemke kwa moto mdogo kwa dakika 5 hadi 10.

Supu yako ipo tayari kwa kuliwa. Na unaweza kuhudumia watu wanne.

Urojo


UROJO ni chakula kilichozoeleka sana Zanzibar,na mara nyingi kimekuwa kikitumiwa sana wakati wa jioni.

Chakula hiki kimekuwa kikiliwa sana hasa wakati wa jioni katika mitaa mbalimbali nchi hasa katika ukanda wa Pwani.

Kutokana na maombi ya wasomaji wengi wakinitaka niwaelezee namna ya kutengeneza upishi huu leo nimeamua kuja nao ili kuwapatia ladha ya kile wanachohitaji.

Urojo hivi karibuni umekuwa ukijulikana kama mix kutokana na mchanganyiko wa vitumbalimbali unaowekwa ili kukmilisha chakula hiki.

Fuatana nami ili ujue namna ya kuandaa chakula hiki chenye ladha ya kipekee

Mahitaji


Mbatata (viazi ulaya) kiasi. Unga wa ngano (1/4 kikombe cha chai) Bizari 1/2 kijiko cha chai (ile ya rangi ya manjano)
Chumvi kiasi. Chatini ya ukwaju
Chatini ya nazi Kababu za kunde au muhogo
Kachori vipande vya figilikrips za muhogo
Namna ya kufanya chukua viazi mbatata osha vizuri weka kwenye sufuria ya maji safi injika jikoni chemsha hadi viive.
Vikishaiva viipue na vitoe kwenye maji kisha vimenye
Vikatekate katika vipande vidogovidogo na weka kwenye bakuli.
Chukua sufuria nyingine weka maji vikombe vinne weka chumvi kijiko kimoja kikubwa
Koroga uji wa unga wa ngano
Hakikisha uji huo unakuwa mwepesi
weka binzari .
Ukishachemka ipua na weka pembeni kwenye bakuli.


Ukishamaliza yote hayo kinachuofuatia ni kuchanganya vitu vyote ulivyonavyo ili kupata urojo halisi.

Chukua bakuli yako yenye ukubwa wa kiasi inapendeza ikiwa ya Kaure.

Weka urojo pawa tatu,kababu za kunde5,kachori 5, kripsi vijiko vitatu vya mezani,viazi mbatata kiasi na mishikaki
Weka chatini ya ukwaju na chatini ya nazi
Halafu katia figili.

Urojo wako tayari kwa kuliwa.

wali wa kichina

mahitaji

Mchele 1 na 1/2 kilo
Kamba wadogo 1kilo (unaweza kutumia kuku aliyechambuliwa au chaza)
Limau/ndimu 1
Carrot 2-3 (osha kata kwa urefu mara 4 ikisha kata slesi)
Njegere 1/2 kilo
Pilipili boga 1(iliyokatwa vipande vidogo)
Yai 1
Viungo kiasi (pilipili manga, uzile, mdalasini, iliki vilivyosagwa)
Vitunguu maji kiasi (kata vya kukaanga na kutwangwa na thomu)
Thomu kiasi (punje 1-2)
Bizari njano kiasi
Mbatata 2-3 (kata ndogo ndogo ukipenda tia)
Maji kiasi
Mayonaise kiasi(ukipenda)
Mafuta kiasi
Chumvi kiasi

Namna ya kupika

Chemsha kitoweo, chumvi, bizari na ndimu hadi kiwive na kiwe kikavu (au na urojo kidogo), chemsha njegere mpaka zisiwive zikawa laini
Twanga thomu, chumvi kidogo, vitunguu maji na viungo vyote
Chemsha wali kwenye maji ya chumvi na uchuje ukiwa una kiini cha kiasi ya kuwiva, weka pembeni
Weka sufuria unayohisi inaweza kuingia vitu vyote, na utie mafuta
Kaanga vitunguu maji kidogo, mbatata, pilipili mboga, carrot na pia vitunguu vilivyotangwa
Unakoroga kwa muda mdogo hadi zionyeshe kuiva, unatia yai na urojo wa kitoweo kidogo (au mayonaise), ikiasha unamimina kitoweo na njegere
Mwisho unamimina wali na unakoroga hadi uchanganyike na halafu unaonja chumvi kwa kulea ikisha unaoka kwa mkaa kiasi ukauke
Baadae unapakua na unaserve kwa saladi

Kamba wa nazi
mahitaji


kamba wabichi 10 mafuta ya kula vijiko 4 vya mezanikitunguu maji 1 tangawizi mbichi iliyosagwa kijiko 1 cha mezanikitunguu saumu kilichosagwa kijiko1 cha chaibinzari ¼ kijiko cha chaiunga wa pilipili ¼ kijiko cha chaikotmiri iliyokatwakatwa kijiko 1 cha mezani.pilipil hoho 1 tui la nazi kikombe cha chai 1limao au ndimu 1.

Namna ya kutengeneza


Menya kamba wako kisha waweke pembeni. chukua kikaango anza kukaanga kitunguu maji,kisha weka saumu na tangawizi endelea kukaanga hadi viwe hudhurungi.kisha weka binzari na unga wa pilipili halafu kotmiri.
Weka maji kidogo ykianza kuchemka weka kamba wako acha wachemke kwa dakika 3 hadi 4 punguza moto kidogo ili viive kwa nafasi.
Baada ya hapo miminia tui la nazi baada ya kuchemka na kupata kiasi cha mchuzi unachohitaji weka kamulia limao au ndimu kisha chumvi.
Kamba wako tayari kwa kuliwa waweza kula na wali ugali au kitafunwa chochote.
Huu ni mlo kwa ajili ya watu wawili.

Kamba wa kukaanga
Kamba ni aina ya samaki wanaopatikana kwenye maji chumvi na pia kwenye mito hasa maeneo yenye delta kama vile mto rufiji .

Samaki hawa wapo wa aina nyingi na hutofautiana kwa majina kulingana na ukubwa wake kwani wapo wadogo zaidi hujulikana kama uduvi,wakubwa kidogo wanafahamika kama dagaa kamba na wakubwa wanaitwa kamba kochi.

Lakini kwa leo nitakupa kidogo kuhusiana na namna ya kukaanga kamba na ukapata kitafunwa kizuri kwa ajili ya kinywaji chako.

Mahitaji

Dagaa kamba ½ kilo
Unga wa dengu ¼ kilo
Chumvi
Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa kijiko 1
Mafuta ya kula ½ lita
Ndimu na pilipili kama unatumia
Masala .


Namna ya kufanya


Chukua dagaa kamba wasafishe wakate vichwa na uwamenye maganda yao na kuwaacha nyama ya ndani .
Waweke katika bakuli na kisha changaya na na viungo vyote tangawizi ,vitunguu saumu ,masala ndimu na pilipili chumvi.
Nyunyizia unga wa dengu katika mchanganyiko huo hadi upate uji mzito .

Chukua karai mimina mafuta weka jikoni na baada ya kuchemka kaanga dagaa wako hadi wawe na rangi chungwa .
Fanya hivyo kwa dagaa wote katika bakuli lako na baada ya hapo kamba wako wapo tayari kwa kuliwa waweza kula wenyewe kama kitafunwa au waweza kula kama kitoweo kwa kula na chakula kingine .

Pweza wa kukaanga
Pweza ni mmoja kati ya samaki wanaopendwa sana na wakaziwa pwani kutokana na utamu wake, pia virutubisho muhimu kwa afya alivyo navyo.

Zipo aina tofauti tofauti ya mapishi ya samaki huyu,yakiwamo yale ya kukaanga ,kuchemshwa na kupata supu na hata kupikwa kama mchuzi.

Wanaume wengi wa pwani hupendelea supu ya pweza kutokana na wingi wake wa virutubisho vya kuongeza nguvu za kiume kwa waliopungukiwa.

Mahitaji

Pweza mbichi nusu kilo
Mafuta ya kupikia ½ lita
Chumvi kijiko 1 cha chakula
Chatini ya ukwaju au pilipili ya kusaga
Maji nusu lita.

Namna ya kutengeneza.


Chukua samaki wako na muoshe vizuri na kumtoa uchafu wote.Muweke katika sufuria,weka chumvi,kisha bandika jikoni acha hadi vichemke na maji ya kwanza yakauke.
Kwa kuwa samaki huyu anasifa ya kuwa na nyama ngumu weka maji yako tena na achemke hadi uhakikishe kuwa ameiva.

Baada ya hapo muopoe na kumeweka kwenye chombo kikavu,kisha weka karai jikoni mimina mafuta na baada ya kupata moto weka pweza wako.

Mkaange hadi awe na rangi ya machungwa kisha mtoe na kumkata kata.

Weka kwenye sahani na pembeni yake weka na kibakuli cha chatni. Pweza wako tayari kwa kuliwa.

Sosi ya nyanyaSOSI ya nyanya ni moja kati ya sosi ambazo zinapendwa na watu wengi, kutokana na ladha yake na pia urahisi katika utengenezaji wake.

Kiasili sosi hii imekuwa ikitumiwa sana na wataliano ambapo wao waifahamu kama ‘pomodoro sauce’na mara nyingi wamekuwa wakila na tambi kwa kuwa ndio chakula chao kikubwa.

Lakini je wajua namna ya kutengeneza soso hii? Kwanza kabisa nataka nikujuze kuwa kuwa hii ni sosi ambayo ni rahisi kutengeneza kuliko zile unazozifahamu.

Mahitaji


Nyanya kubwa 2
Kitunguu maji 1
Karoti 1
Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 cha mezani
Mafuta ya kula vijijiko 3 vya mezani
Majani ya vitunguu
Sukari 2½ kijiko
Chumvi kiasi


Namna ya kutengeneza


Chukua mafuta ya kula weka katika sufuria na kisha weka jikoni, baada ya kuchemka anza kwa kukaanga kitunguu saumu, halafu weka kitunguu maji kaanga kwa dakika moja kisha weka slesi za nyanya zikifuatiwa na majani ya kijani ya vitunguu endelea kukoroga, acha vichemke huku ukikoroga kuzuia visiungue kwa muda wa dakika 10.baada ya kuhakikisha kuwa zimeiva weka chumvi na sukari.
sosi yako ipo tayari kwa kuliwa waweza kula na mkate chapati au hata tambi.

Keki ya Krismasi

Mahitaji

Unga wa ngano robo kilo
Margarine robo kilo
Sukari ya kawaida robo kilo
Mayai sita
Baking powder
Vanila ,hiliki au marashi tone moja
Sukari ya kusaga robo tatu kilo.
Rangi ya kijani njano,kijani na nyekundu.
Mayai mawili
Kipande cha ndimu au limao
Namna ya kupika

Chukua bakuli la plastiki au la udongo
Changanya margarine na sukari hadi iwe na rangi nyeupe na kusagika kabisa .
Weka mayai huku ukiendelea kuchanganya
Weka vanila au hiliki au marashi tone moja
Hakikisha unapatikana uji mzito kutokana na mchanganyiko huo.
Mimina uji huo katika chombo kikavu cha kuokea ,yaweza kuwa cha pembe nne au kama utahitaji keki ya mshumaa au kengele ya kristmas waweza kutumia chombo chenye umbo la duara..

Oka waweza kutumia jiko la mkaa au jiko la umeme au hata gesi hii itategemea uwezo wa mpishi .

Baada ya keki kuiva iache ipoe kwa muda na baada ya hapo shughuli ya kupamba inaanza.

Namna ya kupamba keki

Chukua ute tu katika hayo mayai mawili yaliyobakia
Kamulia kipande cha ndimu
Koroga hadi yakatike na kuwa na rangi nyeupe
Miminia sukari ya kusaga hadi iwe kama ugali mzito.
Gawanya katika vibakuli vingine vitatu kila kimoja weka rangi yake kijani njano na nyekundu na nyeupe .
Baada ya hapo chukua kifaa cha kupambia keki(icing set) na anza kuweka sukari nyeupe na uizungushie katika keki yote.
Kisha nakshi kwa kutumia rangi nyengine ukitengeneza umbo la mshumaa au kengele ya krismas .Keki yako tayari kwa kula

chachandu ya maembe mabichi

Wengi wetu tumekuwa tunahitaji sana pilipili katika kukifanya kutengeneza hamu ya kula chakula lakini tumekuwa tukishindwa kuelewa ni ipi aina bora ya pilpili kwa afya zetu .

hii hapa teknolojia rahisi ya kutengeneza pilipili kwa gharama nafuu na bila kuondoa virutubisho ambavyo ni muhimu kwa afya zetu na vilevile kati.

Mahitaji

Embe aina ya dodo bichi 1
Tangawizi 1 kubwa
Kitunguu saumu 1
Kitunguu maji 1 kikubwa
Tango 1
Pilipili hoho 1
Karoti 1 Chumvi kijiko 1 cha chakula
Nyanya nne kubwa
Pilipili mbuzi za kuiva 10
vinega

Namna ya kutengeneza.

Chukua vitu vyote viweke kwenye bakuli kubwa la plastiki na osha kwa kutumia maji ya moto ili kuhakikisha usafi zaidi .

Menya embe pamoja na viungo vingine vinavyotakiwa kumenywa kisha katakata katika vipande vidogovidogo halafu weka katika mashine ya kusagia na uvisage hadi viwe kama uji mzito .

Hifadhi katika chupa tayari kwa kuliwa ,waweza kula na vyakula kama wali.ndizi au waweza kula kama achali kwa kula na bagia au kababu.

Chatini Ya Ukwaju

Chatini ya ukwaju ni mchanganyiko ambao umebuniwa kwa ufundi mkubwa kwani una harufu na ladha ya kuvutia na hii yote ni katika kufanya chakula kiwe na ladha na hata thamani zaidi .
Ukwaju ni kiungo ambacho ambacho kwa watu wengi wamekuwa wakitumia kama juice tu lakini ni kiungo chenye matumizi mengi kuliko watu wanavyofikiria .

Kwa watu wa pwani hasa katika visiwa vya unguja na pemba ukwaju umekuwa ukitumika kama ndimu katika chakula kwa lengo la kuchangamsha chakula husika.
Vilevile ukwaju umekuwa ukitumika kama vinega kwa kutumika kwenye saladi na mara nyingine hutumika kwenye vyakula vyenye shombo kwa lengo la kukata shombo.

mahitaji
UkwajuTangawizi mbichiPilipili mbichi kiasi unachohitajiKitunguu Saumu kitunguu maji ( si lazima vile )chumvi
(Vipimo itategemea kiasi unachohitaji)

Namna ya kutengeneza

Anza kwa kutwanga vitunguu maji na swaumu.
Changanya na pilipili halafu huku ukiendelea kutwanga hadi vilainike .
Weka chumvi kiasi
Chukua ukwaju menya maganda yake na kamua na kupata rojo nzito .
Changaya pamoja na mchanganyiko huo uliotwanga .
Mpaka hapo chatini yako itakuwa tayari kwa kuliwa waweza kutumia katika chipsi katres pamoja na vitafunwa vingine au waweza kutumia katika mlo kama wali na ugali.

Chatne ya machicha ya nazi
Chatne ni aina ya chachandu yenye asili ya kihindi ,ambayo kazi yake kubwa ni kuongeza hamu ya chakula kama ilivyo kwa aina nyingine za chachandu.

Mara nyingi chatne huliwa na bagia au kachori na pia urojo hasa kwa wale waishio maeneo ya pwani hasa visiwa vya unguja na pemba.

Kuna aina nyingi za chatne kama vile za mapapai ,karoti pamoja na nyinginezo nyingi lakini kama nilivyokueleza mwanzo leo nitakuletea chatne ya nazi.

Mahitaji

Nazi iliyokunwa kikombe 1
Pilipili 3 zilizoiva
Chumvi kijiko kimoja cha chai
Limao au ndimu au hata ukwaju
Pilipili manga za kusaga kijiko kimoja cha chai

Namna ya kutengeneza


Hakikisha nazi unayotumia inakuwa laini na katika hatua ya kwanza unachukua nazi yako
Changanya na pilipili ambayo imesagwa
Weka chumvi halafu
Weka limao ,ndimu au ukwaju .
Changaya pamoja na baada ya hapo weka chumvi pamoja na pilpili manga za kusaga
Baada ya hapo chatne yako itkuwa tayari kwa kuliwa .

Vipopoo

Vipopoo ni upishi ambao unaojulikana sana katika maeneo ya pwani ingawaje mpaka leo haijajulikana asili hasa ya upishi huu.

Naweza kusema haijulikani asili yake kwani upishi huu umekuwa ukipikwa pia na wenyeji wan chi za Japani ,Thailand na maeneo yam engine lakini vikiwa na majina tofauti.

Vipopoo vipo vya aina tatu na vimegawanywa kulingana na aina ya unga unaotumika katika kuvitengeneza.

Waweza kutengeneza vipopoo kwa kutumia unga wa muhogo ,ngano na hata mchele na pamoja na kupisha kutokana na aina ya unga upishi wa vipopoo hivyo ni wa aina moja .

Nasema ni wa aina moja kwani viungo vinavyotumiwa katika upishi huu vinashabihiana kwani kwa kawaida vipopoo huungwa na nazi pamoja na sukari.


Mahitaji

Ungawa mchele 1kg
¼ kijiko cha chai unga wa iliki
tui zito vikombe viwili
½ kikombe cha sukari
maji lita moja
rangi ya chakula


namna ya kutengeneza

weka maji jikoni na yaache ya chemke kama ya ugali na yakishachemka weka unga wa mchele, songa vizuri na mwiko mpaka uwe mgumu kama ugali wa kawaida .
Gawanya katika sehemu mbili au zaidi kutokana na rangi ngapi unatumia.
Ongeza rangi halafu endelea kusonga mpaka uchanganyike vizuri.
Chukua mabonge yako ya unga na yaweke katika ungo wenye unga ili utakapotengeneza visigandane.
Tengeneza vimviringo vidogo vidogo kama vigololi au vyenye ukubwa njugu mawe.
Changanya sukari, kikombe kimoja cha maji, na nazi. Hakikisha sukari imeyayuka kabisa, halafu chemsha.
Weka vimviringo vya mchele kwenye nazi inayochemka, acha vichemke kama dakika tano, ipua.
Weka kwenye vibakuli vya kitindamlo.

chauro

Chauro ni kitafunwa chenye asili ya bara asia kutokana na umaarufu wake wa kulima mpunga pia watu wa bara hilo wamekuwa wabunifu wa mapishi mbalimbali yatokanayo na zao hilo.


Mahitaji


Pepeta ¼
Karanga ¼
Viazi ulaya ¼
Dengu ¼
Chumvi kijiko cha chakula
Sukari kijiko cha chakula
Pilipili ya unga kijiko cha chakula
Mafuta ya kula lita moja

Namna ya kutengeneza

Menya viazi vioshe na vikatekate slesi na kisha weka karai la mafuta jikoni baada ya kuchemka weka viazi na vikaange hadi viive na kukauka, osha karanga na kisha zikaange hadi zikauke osha dengu nazo zikaange baada ya hapo ukivitoa kwenye mafuta vichuje na kisha ziweke hadi zipoe.

Vikishapoa vichanganye na uviweke kwenye chombo chenye nafasi na kikavu halafu nyunyizia sukari kiasi chumvi na pilipili.

Chauro zako tayari kwa kuliwa.

Eggchop


'Eggchop' kitafunwa ambacho hupendwa na watu wengi watoto kwa wakubwa na vilevile hutumika kama chakula maalum katika hafla au sherehe mbalimbali.

Eggchop mara nyingi huwa katika umbo la duara au yai alimradi katika umbo ambalo litakufanya uvutiwe .

Mahitaji

Mkate mmoja
Mayai 10
Chumvi kijiko 1 cha chakula .
Tangawizi kijiko 1 cha chakula
Pilipili manga kijiko 1 cha chai
Kitunguu maji vitatu vikubwa
Kitunguu saumu kijiko cha chakula
Nyama ya kusaga 1/4 kilo

Namna ya kufanya

Chukua mayai 6 yachemshe hadi yaive na baada ya hapo yamenye maganda .
Chukua nyama ya kusaga changanya na tangawizi ,vitunguu saumu chumvi ichemshe hadi ichemke.
Chukua vitunguu maji vichepe katika umbo la boksi
Loweka mkate katika maji hadi uloane kabisa kamua na weka katika bakuli safi na kavu.
Changanya nyama ,vitunguu maji pamoja na mchanganyiko wa mikate .

Chukua mayai manne yaliyobaki yapasue na yaweke katika bakuli weka na chumvi kidogo.

Chukua mchanganyiko wa wako weka katika umbo la miviringo ya chapati kama chukua yai la kuchemsha ingiza katikati ya mviringo huo na kufunika kabisa.

Chovya kwenye bakuli la mayai halafu kaanga kwenye mafuta yaliyochemka kaanga hadi viwe katika rangi ya hudhurungi .
Fanya hivyo kwa mayai yote .

Eggchop zako ziko tayari kwa kuliwa waweza kula kwa soda chai au hata maziwa .

Pudding ya mkate na siagiUpishi wa Puding ni moja kati ya mapishi yanayoweza kupikika kwa urahisi kutokana na upatikanaji wa mahitaji yake.

Mahitaji


Mkate vipande vyembamba 2 au 3
Siagi 2 au3 vijiko vikubwa
Zabibu 1kijiko kikubwa
Maziwa 1kikombe
Yai 1
Vanila kijiko kidogo kimoja
Sukari 3 vijiko vikubwa

Namna ya kutengeneza


Paka siagi ndani ya bakuli.
chukua vipande vyako viwili vya mkate, paka siagi tia zabibu katikati ya vipande hivyo kisha vibane pamoja.
Weka ndani ya bakuli lako la bati
Koroga yai na kulichanganya vizuri pamoja na maziwa, vanila na sukari.
Mimina juu ya mkate katika bakuli .
Oka polepole katika jiko na kupakua ungali umoto.

Pudding yako ipo tayari kwa kuliwa, waweza kula na kinywaji chochote cha baridi.

Katres za nyama ya kusagaKatres zipo za aina nyingi waweza kupika katres za viazi mbatata, samaki ,nyama na hata mayai .

Lakini leo nitakupa kidogo kuhusiana na katres za nyama .

Mahitaji

Viazi mbatata ¼ kilo
Nyama ya kusaga ¼ kilo
Karoti 1 kubwa
Pilipili hoho 1 kubwa
Chumvi kijiko cha chai
Mayai 5
Mafuta kula lita 1
Kitunguu saumu 1
Kitunguu maji 1
Pilipili mbuzi kiasi unachohitaji .
Unga wa ngano ¼ kilo.
Ndimu 1 kama unatumia

Namna ya kufanya

Chukua viazi mbatata vioshe halafu vichemshe na maganda yake ,baada ya kuiva viweke kwenye maji baridi na kisha menya maganda yake.
Chemsha nyama ikiwa imeunwa na tangawizi au ndimu ili kuondoa shombo na kuifanya iive haraka .
Viweke kwenye kinu na uvisage hadi vilainike kisha weka kwenye bakuli .
Chukua hoho na karoti vikate vidogovidogo halafu weka kwenye bakuli la viazi.
Twanga saumu na kitunguu maji kisha changanya kwenye mchanganyiko wako weka na chumvi na kama itakuwa ndogo ongeza kidogo ili kuleta ladha nzuri na ikiwa unatumia ndimu changanya katika mchanganyiko wako huo .
Weka nyama ya kusaga iliyochemshwa na changanya pamoja .

Baada ya hapo waweza kutengeneza matonge yenye umbo la yai huku ukiyapaka unga wa ngano kuzuia yasigande mikononi fanya hivyo kwa mchaganyiko wote ulio kwenye bakuli.
Chukua mayai yavunje na yamimine kwenye bakuli nyingine iliyo kavu na nyunyuzia ngano kidogo na chumvi .
Weka mafuta kwenye karai na anza kukaanga katres zako chukua tonge moja lichovye kwenye mchanganyiko wa mayai na kulizungushia lote kisha weka kwenye mafuta yanayochemka fanya hivyo kwa matonge yote.

Baada ya hapo katres zako zitakuwa tayari kwa kuliwa waweza kula kwa kinywaji chochote iwe ni cha baridi au hata pombe.

ChapatiChapati ni chakula kinachopikwa na kuliwa sana na watu wa Afrika ya mashariki ,Malaysia na kwa kiasi kikubwa nchini India.

Chapati huliwa kama kitafunwa na waweza kutowelea na mchuzi au mboga au kitoweleo chochote.
Kwa kawaida chapati zipo za aina mbili za maji na za kusukuma.chapati za kusukumwa hupendelewa na watu wengi sana. Lakini je unajua zinavyopikwa kama ulikuwa hufahamu angalia hapa chini


Mahitaji


Unga wa ngano vikombe viwili vya chai.
Chumvi nusu kijiko cha chai
Maji ya moto
Mafuta ya kupikia

Jinsi ya kupika


Changanya unga chumvi na maji. Kanda taratibu hadi uwe umelainika weka mafuta kijiko kimoja endeelea kukanda mpaka uhakikishe mafuta yamekolea kwenye unga.kata matonge manne yaliyo sawa katika umbo la mduara kama chungwa na uache kwa dakika chache.
Chukua donge mojamoja weka paka unga kwa nje halafu weka kwenye kibao cha kusukumia na sukuma hadi iwe katika umbo bapa .paka mafuta sehemu ya juu halafu kunja (roll) baada ya hapo zungusha kupata umbo la mdura ili kurahisisha katika kusukuma .
Sukuma tena kupata umbo la bapa halafu weka chuma cha kukaangia chapati jikono baada ya kupata moto weka chapati jikoni na igeuzegeuze mpaka iive weka mafuta kaanga hadi ikupe rangi ya dhahabu.
Fanya hivyo kwa unga wote ulioandaa .
Andaa chapati zako tayari kwa kuliwa .

Mkate wa pasakaMkate wa pasaka ni mkate wenye asili ya kigiriki ambapo,kiutamaduni ulibuniwa maalum kwa ajili ya sikukuu ya pasaka.

Mkate huu hunakshiwa na rangi nyekundu ikiwa ni alama ya kuonyesha kumwagika kwa damu ya yesu ikiwa ni moja kati ya imani zao.

mahitaji


Sukari ¼ kikombe Chumvi kijiko 1 cha chaiHamira kijiko kimoja cha chai
Unga wa ngano ½ kiloMargarine 2 vijiko vya chakula.
Maziwa vikombe viwili vya chaiMayai 9 Unga wa ganda la limao vijiko 2 vya chakulaRangi nyekundu kijiko kimoja
Maji kijiko kimoja cha chai

Namna ya kufanya


Hatua ya kwanza


Chukua bakuli la plastiki lenye ukubwa kiasi changanya unga wa ngano,chumvi sukari,hamira na maziwa.
Kanda unga wako hadi ulainike vizuri kisha uweke pembeni.

Hatua ya pili


chukua maziwa vijiko vitatu, changanya na margarine weka jikoni hadi margarine iyeyuke,kisha weka mchanganyiko huo kwenye mashine ya kuchaganyia changanya taratibu,weka na mayai mawili ambapo yai moja litoe kiini na ubakie ute huku ukuendelea kupiga weka unga wa limao.

Hatua ya tatu


Chukua rangi changanya na maji pamoja na unga wa ngano ili upate uji mwekundu.
Chukua mayai mabichi yapake mchanganyiko huo na kuyafanya yaonekane mekundu.

Baada ya hapo chukua unga wako uliokanda na usuke katika umbo la mkufu
Kisha yapachike mayai katikati ya mkufu huo
Chukua chombo cha kuokea paka mafuta na kisha weka unga wako tayari kwa kuoka.

Oka kwa muda wa dakika 30 au hadi uwe na rangi ya hudhurungi,
Chukua mchanganyiko wako namba mbili paka juu ya mkate wako kabla haujapoa.

Mkate wako tayari kwa kuliwa

Mkate wa kukaanga


mahitaji


dengu zilizochemshwa - 250 gms vitunguu vya kukaanga - 25 gms hoho - 10 gms nyanya - 15 gms limao - 1 Tangawizi kijiko cha chai
Kitunguu saumu kijiko kimoja cha chai masala ya mchuzi – kijiko cha chakula Chaat masala – kijiko cha chakula mkate – silesi 3 slices mafuta ya kula ½ lita

Namna ya kuandaa


kata mkate katika vipande vyenye umbo unalopendelea changanya na juice ya limao na chumvi kiasi ,vikaange katika mafuta yaliyochemka .
vikaange hadi view na rangi ya hudhurungi halafu viopoe.
chukua sufuria kavu weka jikoni weka kijiko kimija cha mafuta kaanga vitunguu maji kisha weka tangawizi na vitunguu saumu.
changanya na nyanya huku ukiendelea kukaanda hadi viive
weka masala pamoja na dengu koroga hadi vichanganyike vizuri vikishachanganyika vizuri ipua
chukua nyanya moja ikate silesi pamoja na vitunguu maji kata katika la mduara umbo andaa

mkate wako katika sahani tayari kwa kuliwa.