Tuesday, August 31, 2010

Ally Remtullah apata shavu Miss TanzaniaMbunifu Mahiri wa mitindo nchini Ally Remtulah amechaguliwa kubuni mavazi maalum ya Miss Vodacom Tanzania 2010.

Saturday, August 28, 2010

Swahili fashion week

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wabunifu wa Tanzania kufundishwa mbinu za biashara kuelekea katika Soko la Uingeraza.
Wanunuzi wakubwa wa bidhaa za ubunifu kutoka Uingereza kuonyesha mbinu za uuzaji.
Swahili Fashion Week kwa kushirikiana na Tanzania Cotton Board (TCB) na Textile Sector Development Unit (TSDU) kwa pamoja wameandaa mafunzo kwa wabunifu wa Tanzania yenye lengo la kuboresha taaluma ya ubunifu hapa nchini.
“Tunaamini kwamba baada ya mafunzo haya, wabunifu wa watanzania wataweza kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ambazo zitaweza kuuzwa sehemu yoyote. Pia kupitia mafunzo haya tunaamini kwamba wabunifu watapata habari muhimu zitakazowawezesha kuchangia moja kwa moja ukuaji wa sekta ya ubunifu Tanzania ”. Alisema Mustafa Hassanali muaandaji wa Swahili Fashion Week.
Mafunzo hayo yataendeshwa na Claire Hamer-Stubbs ambae anatoka katika kampuni ya Ei8ht (www.ei8ht.org), kundi ambalo limekuwa likifanya kazi zake nchini Uingereza.
Warsha hiyo itafanyika katika Hotel ya New Africa kwa muda wa siku nne kuanzia Ijumaa ya tarehe 27 mpaka Jumatau tarehe 30 mwezi huu na kuwahusisha wabunifu 12 wa mavazi hapa nchini.
“TSDU kwa sasa tumeshirikiana na Swahili Fashion Week katika programu ya kuwasaidia wabunifu wa Tanzania kwa kutoa mafunzo ya awali , TSDU inaamini kwamba kwa kutoa fursa ya mafunzo kwa wabunifu ambayo yatawawezesha kutambua mpangilio mzima wa kufanya kazi zao. Tunaamini kwamba kupitia semina hii wabunifu watajipatia uelewa mpana wa kufanya kazi na wanunuzi wa rejareja kutoka Uingereza ambao huenda wakavutiwa na bidhaa zinazozalishwa na wabunifu wa Tanzania . Alieleza Mark Bennet, mtaalamu kutoka viwanda vinavyotengeneza nguo vya hapa Tanzani.

Miongoni mwa maeneo yatakayofundishwa katika warsha hii ni pamoja na:
• Biashara na ubunifu, ambapo zaidi itagusia kufafanua ubunifu, mifano mbalimbali, gharama za uzalishaji.
• Masuala ya uzalishaji kwa ujumla, ambapo zaidi wataangalia vipengele vinavyohusu fedha, ufundi, ubora wa bidhaa na jinsi ya kufanya kazi na viwanda vingine vya uzalishaji.
• Ufundi katika ubunifu kwa mfano katika ufungaji, uwekaji wa lebo, maadili ya uzalishaji sambamba na mazingira ya kazi kwa ujimla.
• Watapata pia fursa ya kukutana na wanunuzi kutoka Uingeraza, na kujua ni bidhaa gani zinazohitajika Uingereza, pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali na jinsi ya kufikia matarajio.

“Wabunifu wa Tanzania waitumie nafasi hii ipasavyo katika kujipatia mbinu tofauti za kutengeneza bidhaa zao, pamoja na kujipatia mbinu mpya za masoko kwa bidhaa wanazozalisha. Nafasi hii haitoi fursa kwa mtu mmoja mmoja bali kwa sekta nzima ya ubunifu hapa nchini.” Alimazia Mustafa Hassanali.

KUHUSU SWAHILI FASHION WEEK
Swahili Fashion Week ni jukwaa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.
“Swahili fashion week in tukio ambalo linawajumuisha wabunifu wakongwe na wale wanaochipukia kuonyesha kazi zao, pia kutoa nafasi kwa wapenzi wote wa sanaa ya mavazi kujumuika pamoja na kufurahia bunifu wa watanzani na kutoka nchi za jirani”. Alifafanua Mustafa Hassanali.
Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kwamba sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa kwa nchi za Afrika Mahariki.
“Kwa mara ya kwanza watu mbalimbali watapata fursa kuuza na kununua bidhaa mbalimbali za Kiswahili kutoka nchi zinazozungumza Kiswahili kama vile vyakula, viatu, nguo na vitu mbalimbali kutoka mwambao wa Kiswahili kupitia Swahili Shopping Festival”. Alimalizia Mustafa.
Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week imekuwa ikifanyika, ambapo kwa mwaka huu itafanyika kuanzia tarehe 4 mpaka 6 November 2010, Dar Es Salaam , Tanzania .

KUHUSU NA UKUAJI WA VIWANDA (TSDU)
The Tanzania Cotton Board’s (TCB) na Textile Sector Development Unit’s (TSDU) zimekua zikisaidia kukuza seka ya viwanda Tanzania . Lengo kuu ni kubuni hali bora na kuhakikisha kukua viwanda vinavyozalisha nguo Tanzania , sambamba na kuhakikisha thamani ya Pamba Tanzania inakua, hali itakayochangia kupatikana kwa nafasi za ajira na kuwepo kwa hali bora kwa nchi ya Tanzania .

KUHUSU TANZANIA GATSBY TRUST (TGT)
The Tanzania Gatsby Trust (TGT - www.gatsby.or.tz) imeanzisha program maalumu ya kusaidia serikali ya Tanzania katika kuhakikisha maendeleo ya viwanda vinavozalisha nguo . miongoni mwa program zake nyingi pia ni kusaidia kukuza hali ya wabunifu wa Tanzania . TGT inaamini kuwa kuimarika kwa sekta ya ubunifu kutachangia kuongezeka kwa ajira Tanzania . Kwa kushirikian ana VETA TGT imeanzisha mafunzo ya wabunifu wa mavazi katika vituo vyake vya mafunzo vilivyopo Dar es salaam. Pia TGT imeamua kufanya kazi na Swahili Fashion Week kwa lengo kukuza hali ya ubunifu Tanzania .

Thursday, August 26, 2010

Pudding ya tende

Mahitaji
Siagi/samli 1/4kg
Sukari 1/4kg
Mayai 2
Tende 1/2kg (iponde)
Unga 1/4kg
Baking powder 1tsp

Namna ya kutengeneza
Saga siagi na sukari mpaka ilainike
Tia yai na tende
Tia unga ulichanganywa na baking powder
Paka samli vibati au dishi
Tia pudding, funika karatasi juu,
Funga uzi na tia ndani ya maji yanayochemka muda wa saa 2 na nusu, kisha epua

Pudding ya chokolate

Mahitaji
Matunda 1(apples/berries)yachemshe
Sukari 1kijiko kikubwa(castor sugar)
Maziwa kidogo,
Mayai madogo 2(yachemshwe)
Unga vijiko vikubwa,
Cocoa 1/2 kijiko kikubwa.
Namna ya kutengeneza
Changanya cocoa pamoja na unga au punguza unga na kutia cocoa.
Pakua pamoja na custard yenye sukari nyingi kidogo.

Icing ya Cake

Mahitaji
Sukari laini 2.5 vikombe
Siagi 1/2 kikombe
Ganda la limau kijiko cha chai
Maji ya limau vijiko viwili vya mezani
Arki 1.5 kijiko cha chai
Namna ya kutengeneza
Saga siagi na sukari hadi mchanganyiko uwe tayari
Tia maji ya limau samli iliyoyeyushwa
Weka juani mpaka mchanganyiko uwe wa maji na tayari kuliwa.

Fagi


Mahitaji

Sukari 1/4 kilo
Siagi 1/2 kilo
Maziwa kiasi
Tui kiasi
Cocoa vijiko 3
Chumvi kiasi

Namna ya kutengeneza Koroga cocoa kwa maji.
Teleka sufuria tia maziwa, cocoa, tui, na sukari.
Baada ya dakika 20 tia kidonge cha chumvi katika maji yabaridi.
Tia ndani ya sufuria na piga mpaka ipoe kidogo.
Tia njugu kisha tia katika bati lililopakwa siagi ikipoa kata.

Jam ya Zabibu

Mahitaji
Zabibu 1/4kg
Sukari 1/2kg
Maji kiasi

Namna ya kutengeneza Kosha zabibu toa kokwa, tia maji na sukari
Teleka na upike mpaka iwe nzito na wacha ipoe
Tia ndani ya chupa (tia ndimu au tangawizi)

Jam ya nanasi

Mahitaji

Nanasi menya kata vipande kiasi cha vikombe 2 vya chai
Sukari kikombe 1
Unga wa tangawizi kiasi

Namna ya kutengeneza
Mimina nanasi na tia sukari na tangawizi kwenye sufuria iliyoko jikoni
Acha vichemke na kuiva, ambapo vitakuwa kama uji mzito
Epua na uwache ipowe na baada ya hapo mimina kwenye chupa

Banana chip cookies

Mahitaji

Siagi 125gm
Unga 1 na 1/3 vikombe
Vanilla essence 1kijiko cha chai
Sukari laini 1/2 kikombe
Yai 1
Ndizi 1 kikombe (kata slices)
Njugu 1/2 kikombe (zilizovunjwa vunjwa)

Namna ya kutengeneza

1) Saga siagi, arki, sukari na yai mpaka ilainike
2) Tia unga, ndizi na njugu changanya mpaka uchanganyike
3) Teka mchanganyiko kwa vijiko 2, fanya ball
4) Panga kwenye treya liliyopakwa mafuta, na juu yake pamba ndizi
5) Oka mpaka viwive

Uji wa maziwa na zabibu

Mahitaji


Unga wa ngano 1/2kg
Zabibu 1/2
Sukari 1/4kg
Maziwa point 1
Iliki kiasi
Arki kiasi

Namna ya kutengeneza

1) Loweka zabibu, zitwange iliki koroga unga katika maji.
2) Chemsha maji, yakiichemka mimina unga koroga huku unatia sukari, chukua zabibu uzifikiche.
3) Mimina maji ya zabibu katika uji koroga.
4) Tia maziwa, iliki Na arki. Acha ichemke ichemke Kwa muda mdogo na huku unakoroga.
5) Halafu epua na andaa.


Chai ya maziwa ya viungo


Mahitaji

Maziwa 1lita
Majani ya chai kiasi (1kijiko cha chai au 1( teabag)
Hiliki/vanilla kiasi
Mdalasini kiasi
Tangawizi kavu kiasi
Karafuu 1

Namna ya kutengenezaWeka maziwa juu ya moto, yakichemka tia majani
Halafu endelea kutia hiliki, mdalasini, tangawizi na karafuu huku unakoroga kwa dakika 2-3
Epua chuja wakati unamimina kwenye buli au chupa ya chai.

Angalia: unaweza kutumia kiungo chochote kimoja na kikawa chai hii.

Juisi ya Karoti/Carot juiceMahitaji


Carrots 3
Maziwa 2.5 gilasi
Sukari kiasi
Maji 1gilasi
Arki kiasi

Namna ya kutengeneza 1) Kata carrots na uweke na maji, toa na ukamue maji
2) Tia maziwa, arki juu yake koroga pamoja na sukari
3) Onja na tayari kwa kunywewa

Juisi ya Bungo


Mahitaji

Bungo 4
Maji 2 Lita (Yaliyochemshwa na kupowa au maji ya chupa)
Sukari 1.5-2 vikombe
Arki (strawberry) kidogo

Namna ya kutengeneza
1) Kata mabungo na yaroweke kwenye nusu lita ya maji au tia ndani ya blender (kokwa za bungo pamoja na maji hadi kwenye alama ya 1lt.
2) Kamua kwa vidole au saga kwa dakika moja tuu (ukiwa hutumii mashine unatumia vidole au mikono tafadhali osha mikono yako kwa sabuni na maji yauvugu uvugu)
3) Kamua mpaka uhakikishe kuwa kokwa hazitoi tena rangi ( kwa ufupi maji mara tatu kwa kutia kwenye blenda na mara nne kwa kutumia mikono)
4) Bakisha nusu lita ya maji kwa kuipika sukari na uchanganye kwenye juice au tia juice na sukari kwenye blender na ukoroge. Ikiwa unapendelea kunywa ikiwa ya baridi si vibaya ukaiweka kwenye jokofu
Mpaka hapo juisi yako itakuwa tayari kwa kunywea.

Monday, August 23, 2010

Kanga Lingarie

Ni collection ya aina yake kutoka kwa mbunifu Farha Sultani 'Fnaaaz'.
Najua wengi wetu tumezoea kutumia nguo za za silk na vitaambaa vingine kama hivyo na kusahau kabisa kama vitambaa vya asili yetu vina nafasi kubwa ya kufanya maajabu ikiwa tu vitafanyiwa kazi.
Hebu cheki!

High waisted pants

Baada ya kuhit katika fashion kwa muda mrefu hususani katika msimu uliopita. Hariem Pants zimeondoka na sasa ni wakati wa High waisted pants.
Ikiwa wewe si mpenzi wa suruali si vibaya ukajichanganya na kuingia katika high waisted skirts.
Ni suruali ambazo zilihit miaka ya 40. Mtindo huo ulikaa kwa muda mrefu kabla ya kutoweka. Kwa kipindi kile ulifahamika kama 'Pekosi'
Hebu mcheki Ciara na wenzake!

Saturday, August 21, 2010

Gabriel azindua nembo yake!

Mbunifu wa mitindo Gabriel ole Mollel/Sakita amezindua Nembo yake itakayofahamika kama Sairim. Ulifanyika mjini Arusha katika hoteli ya Naura Spring Hotel
Mbali na uzinduzi huo, Gabriel alionyesha accessories zake mbalimbali pamoja na mavazi yake ya ubunifu.
Mengi kati ya mavazi yake hayo yametengenezwa kwa kutumia ngozi.
Cheki 'Pure leather outfits'

Kanga jeans katika ulimwengu wa fashion

Katika kuhakikisha anaitangaza vizuri nchi yake. Mbunifu wa mitindo wa kitanzania Vida Mahimbo amekuja na Collection mpya kabisa inayofahamika kama Kanga Jeans.

Kanga jeans kwa mara ya kwanza kabisa ilionyeshwa katika New york Fashion week. Ambapo wadau wengi walionyesha kuikubali collection hiyo.

Kwa kuwa Lengo lake ni kuisambaza dunia nzima. Tarehe 11 ya mwezi huu, Vida mahimbo alionyesha vitu vyake hivyo katika ufukwe Forte Dei Marmi nchini Italia.
Hivi sasa anaazimia kuonyesha ubunifu wake huo nchini. Na kwa kuanzia ataonyesha katika fukwe za Zanzibar . Hapo wadau wa mitindo watapata wasaa wa kujionjea ladha ya mavazi yake hayo.

Unataka kupungua? fanya haya!

Unene kupita kiasi mara nyingi umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa kupoteza muonekano mzuri kwa watu wote.
Kwa kufahamu hilo, leo nimeona si vibaya nikakupa ushauri juu ya namna gani ufanye ili kupunguza uzito na umbo lako kwa ujumla.

1. Usiwe mtumwa wa tabia zako!
Kila mmoja wetu na kijitabia chake kilichojificha. Inawezekana wewe una mazoea ya kula sa choklet na soda mara kwa mara. Unaonaje ukibadilika na kutumia vinywaji vya afya kama vile juice za matunda na maji?.

2. Tembea
Kwa kuwa inafahamika fika kuwa kutokana na majukumu ya kikazi tumekuwa tukikosa muda wa kufanya mazoezi. Unaonaje ukatumia muda wako hususani wakati wa kurudi nyumbani. Tembea kadri ya uwezo wako kwani wakati mwingine husaidia kupunguza uzito wa mwili wako.

3. Angalia mlo wako

Kwa kupunguza kiasi cha chakula unachokula katika mlo wako wa kila siku, utaishi maisha ya raha siku zote. Pia utakuwa ukupungua taratibu.


4. Kula chips zenye mafuta kidogo
Ndio, unaweza kufurahia chips zako kuwa kutengeneza zile zinazotumia mafuta madogo. Badala ya kuaanga chukua viazi vyako na vikatekate silesi pulizia mafuta na kisha oka kwenye oven. Tayari utakuwa umepata chips zisizkuwa na mafuta.

5.Usipunguze milo yako
Kamwe usithubutu kuacha kula milo yako ya kawaida. Kula milo mitatu mikuu na mingine miwili ya nyongeza. Lakini ni muhimu kupunguza mlo wako.
6. Jipe kiu
Weka mazoea ya kunywa maji kila mara. Hata pale unaposikia njaa.

7.Usisahau matunda na mboga za majani

Ni vitu ambavyo vitakufanya ujisikie umeshiba muda wote. Na hivyo kukuacha ukiwa mwenye afya njema.