Saturday, November 21, 2009

Vida Mahimbo, Kibiashara zaidi!Ni mbunifu chipukizi, ambaye analenga biashara ya kimataifa. Pamoja na biashara ameazimia kuitangaza Tanzania kupitia kazi zake
Anatengeneza top za kike, suruali za Denim, mabwanga nguo za kuogele na nguo za ufukweni kwa ujumla n.k
Mwezi uliopita mbunifu huyu alifanya utambulisho wa mavazi na lebo yake, tukio ambalo lilihudhuliwa na wadau na wapenzi wa mitindo nchini na nje ya nchi.

Nyakwesi na 'Painting dress'


Ni mbunifu chipukizi lakini, ana kipaji kikubwa katika ubunifu wake kwani ameaumua kuja kivingine kwani badala ya kutumia Kanga, Vitenge yeye ameamua kuja na 'Painting dress'.

Swahili fashion week
Ni wiki ya mitindo ya kiswahili, iliyofanyika jijini Dar es salaam
Wiki hii iliratibiwa na mbunifu Mustafa Hassanali, ambapo zaidi ya wabunifu 20 kutoka Afrika walipanda Jukwaani.
Kwa upande wa Tanzania wiki hiyo iliwakilishwa Manju Msitta, Ailinda Sawe, FarouqueAbdela Farha Naaz na Kemi Kalikawe.
Wengine ni Virginia Njumba, Christine Mhando Khadija Mwanamboka, Zamda George, Robi Morro, Fatma Amour pamoja na wabunifu wengine kutoka Tanzania Mitindo House.
Uganda iliwakilishwa na Dorothy Lubega ambapo Kenya iliwakilishwa na Vaishali Morjaria, Vera Vee pamoja na John Kaveke.
Msumbiji iliwakilishwa na Adelia na Sheila Tique. Pia alikuwepo David Tlale kutoka Afrika ya Kusini.