Sunday, June 1, 2008

Eggchop


'Eggchop' kitafunwa ambacho hupendwa na watu wengi watoto kwa wakubwa na vilevile hutumika kama chakula maalum katika hafla au sherehe mbalimbali.

Eggchop mara nyingi huwa katika umbo la duara au yai alimradi katika umbo ambalo litakufanya uvutiwe .

Mahitaji

Mkate mmoja
Mayai 10
Chumvi kijiko 1 cha chakula .
Tangawizi kijiko 1 cha chakula
Pilipili manga kijiko 1 cha chai
Kitunguu maji vitatu vikubwa
Kitunguu saumu kijiko cha chakula
Nyama ya kusaga 1/4 kilo

Namna ya kufanya

Chukua mayai 6 yachemshe hadi yaive na baada ya hapo yamenye maganda .
Chukua nyama ya kusaga changanya na tangawizi ,vitunguu saumu chumvi ichemshe hadi ichemke.
Chukua vitunguu maji vichepe katika umbo la boksi
Loweka mkate katika maji hadi uloane kabisa kamua na weka katika bakuli safi na kavu.
Changanya nyama ,vitunguu maji pamoja na mchanganyiko wa mikate .

Chukua mayai manne yaliyobaki yapasue na yaweke katika bakuli weka na chumvi kidogo.

Chukua mchanganyiko wa wako weka katika umbo la miviringo ya chapati kama chukua yai la kuchemsha ingiza katikati ya mviringo huo na kufunika kabisa.

Chovya kwenye bakuli la mayai halafu kaanga kwenye mafuta yaliyochemka kaanga hadi viwe katika rangi ya hudhurungi .
Fanya hivyo kwa mayai yote .

Eggchop zako ziko tayari kwa kuliwa waweza kula kwa soda chai au hata maziwa .

No comments:

Post a Comment