Sunday, June 1, 2008

Urojo


UROJO ni chakula kilichozoeleka sana Zanzibar,na mara nyingi kimekuwa kikitumiwa sana wakati wa jioni.

Chakula hiki kimekuwa kikiliwa sana hasa wakati wa jioni katika mitaa mbalimbali nchi hasa katika ukanda wa Pwani.

Kutokana na maombi ya wasomaji wengi wakinitaka niwaelezee namna ya kutengeneza upishi huu leo nimeamua kuja nao ili kuwapatia ladha ya kile wanachohitaji.

Urojo hivi karibuni umekuwa ukijulikana kama mix kutokana na mchanganyiko wa vitumbalimbali unaowekwa ili kukmilisha chakula hiki.

Fuatana nami ili ujue namna ya kuandaa chakula hiki chenye ladha ya kipekee

Mahitaji


Mbatata (viazi ulaya) kiasi. Unga wa ngano (1/4 kikombe cha chai) Bizari 1/2 kijiko cha chai (ile ya rangi ya manjano)
Chumvi kiasi. Chatini ya ukwaju
Chatini ya nazi Kababu za kunde au muhogo
Kachori vipande vya figilikrips za muhogo
Namna ya kufanya chukua viazi mbatata osha vizuri weka kwenye sufuria ya maji safi injika jikoni chemsha hadi viive.
Vikishaiva viipue na vitoe kwenye maji kisha vimenye
Vikatekate katika vipande vidogovidogo na weka kwenye bakuli.
Chukua sufuria nyingine weka maji vikombe vinne weka chumvi kijiko kimoja kikubwa
Koroga uji wa unga wa ngano
Hakikisha uji huo unakuwa mwepesi
weka binzari .
Ukishachemka ipua na weka pembeni kwenye bakuli.


Ukishamaliza yote hayo kinachuofuatia ni kuchanganya vitu vyote ulivyonavyo ili kupata urojo halisi.

Chukua bakuli yako yenye ukubwa wa kiasi inapendeza ikiwa ya Kaure.

Weka urojo pawa tatu,kababu za kunde5,kachori 5, kripsi vijiko vitatu vya mezani,viazi mbatata kiasi na mishikaki
Weka chatini ya ukwaju na chatini ya nazi
Halafu katia figili.

Urojo wako tayari kwa kuliwa.

No comments:

Post a Comment