Sunday, June 1, 2008

Keki ya Krismasi

Mahitaji

Unga wa ngano robo kilo
Margarine robo kilo
Sukari ya kawaida robo kilo
Mayai sita
Baking powder
Vanila ,hiliki au marashi tone moja
Sukari ya kusaga robo tatu kilo.
Rangi ya kijani njano,kijani na nyekundu.
Mayai mawili
Kipande cha ndimu au limao
Namna ya kupika

Chukua bakuli la plastiki au la udongo
Changanya margarine na sukari hadi iwe na rangi nyeupe na kusagika kabisa .
Weka mayai huku ukiendelea kuchanganya
Weka vanila au hiliki au marashi tone moja
Hakikisha unapatikana uji mzito kutokana na mchanganyiko huo.
Mimina uji huo katika chombo kikavu cha kuokea ,yaweza kuwa cha pembe nne au kama utahitaji keki ya mshumaa au kengele ya kristmas waweza kutumia chombo chenye umbo la duara..

Oka waweza kutumia jiko la mkaa au jiko la umeme au hata gesi hii itategemea uwezo wa mpishi .

Baada ya keki kuiva iache ipoe kwa muda na baada ya hapo shughuli ya kupamba inaanza.

Namna ya kupamba keki

Chukua ute tu katika hayo mayai mawili yaliyobakia
Kamulia kipande cha ndimu
Koroga hadi yakatike na kuwa na rangi nyeupe
Miminia sukari ya kusaga hadi iwe kama ugali mzito.
Gawanya katika vibakuli vingine vitatu kila kimoja weka rangi yake kijani njano na nyekundu na nyeupe .
Baada ya hapo chukua kifaa cha kupambia keki(icing set) na anza kuweka sukari nyeupe na uizungushie katika keki yote.
Kisha nakshi kwa kutumia rangi nyengine ukitengeneza umbo la mshumaa au kengele ya krismas .Keki yako tayari kwa kula

No comments:

Post a Comment