Sunday, June 1, 2008

Supu ya uyoga

SUPU ya uyoga ni maarufu sana na inapendwa na watu wengi. Na mara nyingi upikaji wake unatofautiana na kulingana na matakwa ya walaji.

Katika mapishi leo hii nitakuletea namna ya kupika supu ya uyoga na maziwa upishi ambao ni adimu sana kwa walaji walio wengi.

Mahitaji

Uyoga ¼
Unga wa ngano kijiko cha chakula
Margarine (blue band) kijiko cha chakula
Maziwa kikombe kimoja cha chai
Kitunguu saumu viwili vikubwa
Tangawizi mbili kubwa
Chumvi. kiasi

Namna ya kupika

Chukua uyoga wako usafishe na kisha katakata vipande vidogovidogo, halafu kitunguu maji katakata weka kwenye sufuria,chukua tangawizi na kitunguu saumu twanga changanya pamoja, weka chumvi halafu tia lita mbili za maji katika sufuria hilo na kisha chemsha kwa muda wa dakika 20.
Acha ichemke hadi ibakie ujazo wa lita moja au moja na nusu.
Pasha margarine au siagi kaaanga unga wa ngano mkavu hadi ubadilike rangi na kuwa brown, weka maziwa huku ukikoroga.
Endelea kukoroga kwa muda wa dakika 2 hadi 3 kisha weka mchanganyiko uliochemsha awali na endelea kukorga hadi vichanganyike vizuri.
Acha vichemke kwa moto mdogo kwa dakika 5 hadi 10.

Supu yako ipo tayari kwa kuliwa. Na unaweza kuhudumia watu wanne.

No comments:

Post a Comment