Sunday, June 1, 2008

Pweza wa kukaanga
Pweza ni mmoja kati ya samaki wanaopendwa sana na wakaziwa pwani kutokana na utamu wake, pia virutubisho muhimu kwa afya alivyo navyo.

Zipo aina tofauti tofauti ya mapishi ya samaki huyu,yakiwamo yale ya kukaanga ,kuchemshwa na kupata supu na hata kupikwa kama mchuzi.

Wanaume wengi wa pwani hupendelea supu ya pweza kutokana na wingi wake wa virutubisho vya kuongeza nguvu za kiume kwa waliopungukiwa.

Mahitaji

Pweza mbichi nusu kilo
Mafuta ya kupikia ½ lita
Chumvi kijiko 1 cha chakula
Chatini ya ukwaju au pilipili ya kusaga
Maji nusu lita.

Namna ya kutengeneza.


Chukua samaki wako na muoshe vizuri na kumtoa uchafu wote.Muweke katika sufuria,weka chumvi,kisha bandika jikoni acha hadi vichemke na maji ya kwanza yakauke.
Kwa kuwa samaki huyu anasifa ya kuwa na nyama ngumu weka maji yako tena na achemke hadi uhakikishe kuwa ameiva.

Baada ya hapo muopoe na kumeweka kwenye chombo kikavu,kisha weka karai jikoni mimina mafuta na baada ya kupata moto weka pweza wako.

Mkaange hadi awe na rangi ya machungwa kisha mtoe na kumkata kata.

Weka kwenye sahani na pembeni yake weka na kibakuli cha chatni. Pweza wako tayari kwa kuliwa.

1 comment:

  1. sana kwa maarifa mazuri kuhusu pweza.

    Naomba anayefahamu anijulishe hapa Dar es Salaam, wilaya ya kinondoni, ni hoteli au mikahawa gani ambapo pweza wanapikwa kwa ukawaida.

    ahsanteni sana,
    Hussein ( Sinza kwa remi)

    ReplyDelete