Tuesday, October 9, 2012

ABAYA FASHION SHOW YATAKA WADAU WA KIKE KUTUPIA HIJAB KATIKA ONESHO LAO LA MAVAZIColor combo pia itaruhusiwa ili mradi tu hijjab ihusike.
Hivi pia itahusika, you can see it is stylish and descent.
Kwa siye tusioweza kuacha kuvaa skin jeans every friday tutatoka kihiviiiiiii.
Mbona shwari tu, juu ya kisuti chako piga mtandio kimtindo kama huyu mwenzetu.
Jamillah looks sexy and descent.
 Wapenda Ubunifu wa mitindo, Wageni na Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaopenda kuona mitindo mipya ikionyeshwa na walimbwende, wametakiwa wasisite kujitupa katika onyesho la mavazi la Abaya Fashion Show.
Onyesho hilo litaambatana na hafla ya chakula cha mchana itakayofanyika  Ijumaa ya tarehe 12, mwezi Octoba katika ukumbi wa Red Onion uliopo Haidery Plaza.
Hafla hiyo itafanyika kuanzia saa Saa 9 Alasisi hadi Saa 12 jioni na inatazamiwa kuonyesha ubunifu wa kuvutia wa kila aina ya nguo..
Mpenda mitindo yeyote anayetaka kuona ubunifu wa nguo hizo ataushuhudia hapo hapo kwenye onyesho la mitindo na anaruhusiwa kununua kadri zitakavyo onyeshwa.
Katika Maonesho hayo kutakuwepo na burudani kutoka kwa B 52 na Belly Dancers kwa kiingilio cha shilingi elfu 25 pamoja na chakula.
Vazi la Kutokezeya ni Hijjab. “Wear it Your Way!!!!!!!!!!!!!!!!”

No comments:

Post a Comment