Thursday, August 16, 2012

Make up tips kwa ngozi nyeusi

Je, wewe ni mweusi na ungependa kujipodoa? Zipo njia kadhaa ambazo ukizitumia zitakurahisishia zoezi hilo. Je ungependa kuzifahamu? Soma hapa: Nimekuandalia tips zangu nane muhimu za kujipodoa ambazo ukizitumia zitaiacha ngozi yako ikiwa ya kuvutia. Epuka kujikandika rangi za mdomo
Rangi yam domo ni kipodozi muhimu sana kwa mwanamke. Kwa mwanamke mwenye ngozi nyeusi ni vyema ukawa makini na upakaji wa rangi ili asije kuharibu muonekano wako. Pakaa rangi nyepesi ambayo itaonyesha vizuri mipaka ya midomo yako badala ya kukufanya uoenakane kituko. Tumia ‘blushes’ zenye rangi iliyokoza
Angalia makini rangi ya ngozi yako, kisha katika vipodozi vyako chagua blush ilikolea zaidi ya ngozi yako. Kwangu mimi blush ni miongoni mwa vipodozi muhimu katika make up kit yangu. Blush humpendeza mwanamke mwenye aina yeyote ya ngozi cha msingi tu ni kuzingatia dondoo hii muhimu. Cheza na ‘eye shadow’
Ni kweli kabisa kuwa unapokuwa na ngozi nyeusi wakati mwingine inachangaya kupata eye shadow inayoendana na ngozi yako. Hivyo ndio maana nakusahuri kujaribu rangi tofautitofauti ili kupata ile hasa unayoendana nayo. dondoo hii ni muhimu sana ingawaje wanawake wengu huona kama kichekesho. Usisahau poda
Hakikisha unapakaa poda usoni mara baada ya kujipodoa. Hii itasaidia kuondoa hali ya mng’ao katika uso wako na kuuacha ukiwa na rangi bomba zaidi. Jambo la kuzingatia ni kuhakikisha unapata rangi zinazoendana na ngozi yako. Pakaa ‘concealer’ kuficha madoa
Dondoo nyingine muhimu ya kujipodoa kwa wenye ngozi nyeusi ni kuficha madoa na makovu yaliyopo kwenye usoni. ‘Concealer’ ndio njia rahisi ya kuficha madoa hayo kwani huficha na pia kung’arisha ngozi yako na kuiacha ikiwa kama halisi. Unachotakiwa ni kutafuta ile inayoendana na rangi halisi ya ngozi yako. Linganisha rangi zako
Cheza na rangi huku ukihakikisha kuwa zinalingana na zinaendana. Elewa kuwa utakapokoleza sehemu moja halafu ukainyima nyingine utajiweka katika hatari ya kuharibu muonekano wako. Tumia vipodozi bora
Wazungu wanasema ‘The higher the quality, the better makeup’. Ikiwa unahitaji kuonekana vizuri zaidi, ni vyema ukatumia vipodozi bora pia kwani uziri wa vipozi hivi huwa vina uwezo mkubwa wa kudumu muda mrefu tofauti na vile vya ubora hafifu. Usisahau nyusi
Iwe unatumia wanja ama tweezer hakikisha unazikumbuka nyusi zako! Haya wapendwa wangu najua mmezielewa vizuri dondoo zangu hizi za kujipodoa kwa wenye ngozi nyeusi ambazo zitasaidia kukufanya uonekane bomba!

No comments:

Post a Comment