Friday, March 2, 2012

Mapishi


Mahitaji
Margarine, mafuta ya mgando ya nazi ¼ kikombe cha chai
Unga wa kakau (Cocoa Powder) ¼ kikombe cha chai.
Karanga au korosho ¼ kikombe cha chai
Sukari ¼ kikombe
Jinsi ya kutengeneza
Yeyusha mafuta yako hadi yawe ya maji kabisa , weka unga wa kakau, weka sukari koroga hadi vichanganyike, endelea kukoroga ili kuzuia visigande.
Weka karanga au korosho kiasi unachohitaji.

Baada ya hapo imimine kwenye sahani au trei ya bati kisha weka kwenye jokofu kwa muda wa dakika kumi au zaidi.
Ikishapoa itoe katika jokofu na kisha iweke kwenye chombo kwa ajili ya kuikata, hakikisha unatumia karatasi aina ya foil ili kuiweka sawa.tayari kwa kuikata.

Ukishamaliza unatakiwa kuiweka kwenye jokofu kwa ajili ya kuigandisha na kupata ugumu unaohitajika.
Inapendeza kuliwa wakati wa jioni hasa mnapokuwa katika mapunziko ya kawaida.

No comments:

Post a Comment