Monday, March 12, 2012

Fashion tips

Vazi la jioni kwa mwanamke mnene
Kwa kawaida kila umbo huendana na vazi la ina yake. Hivyo ni vyema ukawa makini katika hilo. Ikiwa wewe ni mnene lakini huna tumbo kubwa unaweza kutumia gauni kama vazi lako la kutokea wakati wa jioni. Ingawaje mambo huwa ni tofauti kidogo kwa wale wenye matumbo makubwa. Kwani wanawake wa aina hii hushauriwa kutumia mavazi ya vipande viwili nikimaanisha sketi na blauzi. Kwa kuvaa mavazi ya aina hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya tumbo lako lisionekane sana. Ukiachilia mbali suala tumbo, kiungo kingine unachopaswa kuzingatia wakati wa kufanya uchaguzi wa mavazi yako ya jioni ni maziwa. Ikiwa una maziwa makubwa unashauriwa kupendelea kuvaa magauni ama blauzi zenye shingo ya v. Kwani kwa kiasi kikubwa kuchangia kuficha ukubwa wa maziwa yako. Na ikiwa una maziwa madogo, unaweza kuvaa hata vazi lilobuniwa na shingo ya aina nyingine ingawaje wataalamu wanadai kuwa mavazi yenye mtindo wa shingo ya duara huchangia kukufanya uonekane mnene zaidi. Kwa upande wa’ hips’ mambo huwa ni hivyo hivyo kwani kwa wale wanawake wenye hips huakiwa kuvaa mavazi yatakayoficha ‘ hips’ zao tofauti na wale wasio na hips. Kwani wao hutakiwa kuvaa mavazi yenye uwezo wa kuwajaza katika maeneo hayo. Zipo njia za kitaalamu ambazo zikitumika ipasavyo, basi mwanamke anaweza kujitengeneza kwa kadri awezavyo. Kwa upande wa mavazi haya ya usiku unaweza kucheza na rangi na kufanikiwa kuboresha muonekano wa umbo lako. Kwa kawaida rangi zina tabia zake. Kwa upande wa mavazi, inaaminika kuwa rangi za kuonekana zina uwezo mkubwa wa kukuza umbo la mtu na kwa upande mwingine rangi za giza zina uwezo wa kupunguza umbo na kuonekana mwembamba kuliko umbo lake halisi. Kwa mangiki hiyo, kwa wanawake wenye hips kubwa ili uonekane uko bomba zaidi unashauriwa kuvaa mavazi yenye rangi za giza kama vile nyeusi, ugolo n.k na kwa wale wenye hips ndogo basi ni vyema wakachagua kuvaa mavazi yenye rangi mchanganyiko. Itapendeza zaidi ikiwa rangi nyeusi ikavaliwa juu na nyeupe au ya rangi ya kuonekana kuvaliwa kwa chini. Hii itasaidia kukufanya uonekane mwenye umbo la kuvutia hasa katika mavazi yak ohayo ya jioni.

No comments:

Post a Comment