Friday, September 4, 2009

MJ kuzikwa leo


Hatimaye Mfalme wa Pop,Michael Jackson,anatarajiwa kuzikwa leo huko Forest Lawn-Glendale,California katika makaburi yajulikanayo kama Holly Terrace.Mazishi yanatarajiwa kuanza saa moja usiku kwa saa za California.
Kwa mujibu wa taarifa kuhusu mazishi hayo,yatakuwa ni mazishi “private” na hivyo ni ndugu,jamaa na marafiki wa karibu pekee watakaoweza kuhudhuria.

Mazishi hayo yanafanyika baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kina wa kifo chake.

Hivi karibuni Mchunguzi wa vifo wa California,alithibitisha kwamba Michael Jackson alifariki dunia kutokana na kuchomwa sindano ya kupunguza maumivu ambayo ilikuwa na dozi kubwa kuliko kawaida. Daktari aliyekuwa naye siku hiyo,Dr.Murray, ndiye anatupiwa lawama zote ingawa mpaka leo hakuna mashtaka rasmi kuhusiana na kifo cha mwanamuziki huyo.


KALALE PEMA PEPONI MICHAEL JOSEPH JACKSON

No comments:

Post a Comment