Saturday, May 31, 2008

Mkate wa mayai





Karibu mpenzi msomaji wangu katika safu hii ya mapishi kama ilivyoada kila wiki ninakuletea namna ya kupka aina ya upishi ambao natumai utakupendeza .

Kwa leo nakuletea namna ya kupika mkate wa mayai wa kukunja uluonakshiwa na jam.

Wengi watu tumezoea kula mikate ya kawaida kama vile mkate wa kumimina, mkate wa skonsi na mkate wa boflo lakini mkate wa mayai wa kukunja umekuwa kitu kigeni miongoni mwa watanzania wengi.

Mahitaji
Mayai 6
Sukari vijiko3 vya chakula
Unga wa ngano vijiko 3 vya chakula
Maziwa ya unga vijiko 3
Vanila
Foil
Margarine
Jam
Unga wa soda ½ kijiko cha chai

Namna ya kufanya

Chukua bakuli kavu la plastiki au la kaure
Pasua mayai yote na yamimine katika bakuli weka unga wa soda kisha yapige hadi yatike povu jeupe .
Changanya na sukari huku ukiendelea kukoroga,weak maziwa ,weka unga wa ngano margarine kijiko 1 kikubwa cha chakula,vanilla matone matatu.
Endelea kukoroga hadi upate uji mzito.

Uache mchanganyiko huo kwa muda wa dakika tano huku ukiandaa moto kwa ajili ya kuoka mkate wako .

Andaa trei lenye umbo la pembe nne kwa ajili ya kuoka mkate wako , chukua karatasi la foil na litandaze kwenye trei hiyo.
Mimina mchanganyiko huo na kisha usambaze juu ya foil
Oka kwa moto usio mkali sana .
Baada ya kuiva toa ndani ya jiko na paka jam kwa upande wote wajuu.
Baada ya hapo ikunje (roll) huku ukiondoa foil na kuiacha ilivyo.
Mkate wako tayari kwa kuliwa ,unashauriwa kuweka ndani ya jokofu ili kuufanya upoe na kuleta ladha nzuri zaidi.

Waweza kuliwa na kinywaji chochote cha baridi.

No comments:

Post a Comment