Thursday, March 15, 2012

Trend Alert

Shiffon Cape... ikibidi jikepishe bibieee......!

Tuesday, March 13, 2012

Tunic blouse

Katika ulimwengu wa mavazi, kuna mitindo mingi ambayo imekuwa ikishamiri na baadaye kupotea. Lakini kwa wakati huu vazi ambalo limeshamiri ni ‘TUNIC’ambalo lipo katika aina mbili, ambazo ni ‘tunic’ blauzi na magauni. Katika makala hii tutaangalia blauzi za tunic, ambazo kwa sasa zipo katika chati, sio tu hapa nchini bali duniani kwa ujumla. Tofauti na nyingine aina hii ya blauzi huwa ni ndefu na inayoziba sehemu ya ‘hips’ na kuishia kwenye magoti. Pamoja na kuwakubali wanawake wengi, aina hii ya blauzi ni miongoni mwa mavazi mahsusi kwa watu wenye maumbo makubwa. Kwani kutokana na muundo wake huwapa nafasi wavaaji kuziba baadhi ya sehemu za maumbo yao hususan ‘hips’.
Si hivyo tu wakati mwingine tunic hupendeza zaidi pale zinapovaliwa na wajawazito kwani huwafanya wajisikie huru wakati wote. Aina hii ya blauzi, zimebuniwa katika nakshi mbalimbali zikiwamo za rangi moja. Watumiaji wa vazi huusifia mtindo huu kutokana na sifa yake ya kuweza kuvaliwa katika matukio na wakati wowote. Wakati mwingine hutumika kama vazi la kawaida. Lakini ikiwa mvaaji husika ataongeza baadhi ya mapambo huweza kulipa hadhi na zaidi na kuweza kuvaliwa hata kwenye mitoko mbalimbali. Kwa upande wa hali ya hewa, aina hii ya blauzi ina sifa ya kuvaliwa katika misimu mbalimbali. Ikiwa utavaa wakati wa joto, unaweza kuvaa yenyewe kama ilivyo. Lakini ikiwa itavaliwa wakati wa baridi, unaweza kuvaa na blauzi nyingine kwa ndani hususani yenye mikono mirefu.
Ikiwa uko kwenye maeneo yenye baridi sana, si vibaya ikiwa utatumia ‘pull neck’. Kwa upande wa viatu, tunic huvaliwa na viatu vya aina mbalimbali kutegemea na mahali unapokwenda na shughuli unayokusudia kufanya. Ikiwa upo kwenye matembezi ya jioni unaweza ukavaa aina hii ya blauzi na leggings ama ‘skinny jeans’ na kutupia viatu aina ya makubadhi au ‘gladiators’. Jambo la msingi, unalotakiwa kuzingatia, ni umbo lako na rangi ya blauzi hizo. Kama una umbo kubwa sana unashauriwa kutumia mavazi yenye rangi ya giza na ukiwa umbo dogo vaa yale yenye rangi za kuwaka. Hii husaidia kuboresha muonekano wako.

Monday, March 12, 2012

Kiafrika zaidiiiiiiii

Sofa za kitengeeeee !!!!!!!!!!!!!

Nani ameipatia?

Warda
Bi dada

Trend alert.......

Bandage dress Unaweza kujiblazia ukatoka bomba zaidi

Fashion tips

Vazi la jioni kwa mwanamke mnene
Kwa kawaida kila umbo huendana na vazi la ina yake. Hivyo ni vyema ukawa makini katika hilo. Ikiwa wewe ni mnene lakini huna tumbo kubwa unaweza kutumia gauni kama vazi lako la kutokea wakati wa jioni. Ingawaje mambo huwa ni tofauti kidogo kwa wale wenye matumbo makubwa. Kwani wanawake wa aina hii hushauriwa kutumia mavazi ya vipande viwili nikimaanisha sketi na blauzi. Kwa kuvaa mavazi ya aina hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya tumbo lako lisionekane sana. Ukiachilia mbali suala tumbo, kiungo kingine unachopaswa kuzingatia wakati wa kufanya uchaguzi wa mavazi yako ya jioni ni maziwa. Ikiwa una maziwa makubwa unashauriwa kupendelea kuvaa magauni ama blauzi zenye shingo ya v. Kwani kwa kiasi kikubwa kuchangia kuficha ukubwa wa maziwa yako. Na ikiwa una maziwa madogo, unaweza kuvaa hata vazi lilobuniwa na shingo ya aina nyingine ingawaje wataalamu wanadai kuwa mavazi yenye mtindo wa shingo ya duara huchangia kukufanya uonekane mnene zaidi. Kwa upande wa’ hips’ mambo huwa ni hivyo hivyo kwani kwa wale wanawake wenye hips huakiwa kuvaa mavazi yatakayoficha ‘ hips’ zao tofauti na wale wasio na hips. Kwani wao hutakiwa kuvaa mavazi yenye uwezo wa kuwajaza katika maeneo hayo. Zipo njia za kitaalamu ambazo zikitumika ipasavyo, basi mwanamke anaweza kujitengeneza kwa kadri awezavyo. Kwa upande wa mavazi haya ya usiku unaweza kucheza na rangi na kufanikiwa kuboresha muonekano wa umbo lako. Kwa kawaida rangi zina tabia zake. Kwa upande wa mavazi, inaaminika kuwa rangi za kuonekana zina uwezo mkubwa wa kukuza umbo la mtu na kwa upande mwingine rangi za giza zina uwezo wa kupunguza umbo na kuonekana mwembamba kuliko umbo lake halisi. Kwa mangiki hiyo, kwa wanawake wenye hips kubwa ili uonekane uko bomba zaidi unashauriwa kuvaa mavazi yenye rangi za giza kama vile nyeusi, ugolo n.k na kwa wale wenye hips ndogo basi ni vyema wakachagua kuvaa mavazi yenye rangi mchanganyiko. Itapendeza zaidi ikiwa rangi nyeusi ikavaliwa juu na nyeupe au ya rangi ya kuonekana kuvaliwa kwa chini. Hii itasaidia kukufanya uonekane mwenye umbo la kuvutia hasa katika mavazi yak ohayo ya jioni.

Bi mkubwa mie

Moyo Zoo Lake- Johannesburg naikumbukaje?

Saturday, March 10, 2012

Designer spotlight..........

Pooja is the name behind the label Saffron designs. Saffron designs is a ready to wear line of clothing created to express a bold, confident and graceful style found in its every detail & style. Saffron Designs has its foundation in the African patterns. Pooja has enhanced these African patterns with a mix of contemporary designs that has become the style of women both in Africa and internationally. Her unique cuts, shapes, and color has become the fashion frame of reference for women everywhere especially young African women.

Jamani siku ya wanawake kila mwanamke aliadhimisha kivyake...............

TWAA waliadhimisha kwa chai..... shuguli nzima ilikuwa Serena Hotel
Mkurugenzi wa TWAA Irine Kiwia akitoa mawili matatu tembelea www.8020fashion upate uhondo zaidi (juu).
8020fashions ikishirikiana na Bi Khadija Mwanamboka wao walisherehekea kwa kwenda kituo cha KIWOHEDE. Bi mkubwa Shamim akimaliza kazi aliyoianza miezi kadhaa iliyopita kwa kukabidhi vyerehani kwa vijana wa Kiwohede. Wanawake na maendeleo.......tusonge mbele..... Tembelea www.8020fashions.blogspot.com ujionee mwenyewe

Wednesday, March 7, 2012

TWAA Mentorship Program

Nikiwa ofisni jana, nimebahatika kupata mwaliko wa sherehe nyingine ya wanawake. Tofauti na nyingine nilizohudhuria hii itakuwa ni breakfast, ambayo itatujumisha pamoja wadau katika hoteli ya Serena. Nimefurahi sana kupata nafasi hii . Nitawaletea yaliyojiri kwenye sherehe hiyo>>>>>. Wanawake mpooooooooooooooo

Martin Kadinda na campaign yake ya 'single button' inakuja hivi karibuni

Ngozi Anyiam to represent Nigeria

Legendary Models, a subsidiary of Legendary Gold Limited presents Ngozi Anyiam for one of the World's most glamorous events – the 19th Top Model of the World Contest scheduled for the 10th of March, 2012 at the prestigious Westspiel Casino, Dortmund-Hohensyburg, Germany where Top Model of the World Contest will be presenting the most stunning top models from around the world. Ngozi Anyiam will be amongst the 44 stunning contestants from around the world who will converge in Germany to vie for the most coveted title in the Modeling industry. The models will be treated to an exciting and unforgettable tour of various cities before the event proper on the 10th of March. Legendary Gold Limited owns the franchise of Top Model of the World in Nigeria. It undertakes a national model search all over Nigeria annually through its event; The Nigeria Model Awards and it is from The Nigeria Model Awards that Legendary Models recruits its models.
Picha zaidi tembelea kabelelejr.blogspot.com

Mustafa Hassanali in Arise Magazine Fashion Week 2012

Mustafa Hassanali to unveil the ‘Afrikalos’ collection in Lagos, Nigeria Second time for Mustafa Hassanali to showcase in Arise Magazine Fashion Week. The renowned pan African designer, Mustafa Hassanali, is among 77 fashion designers from six continents of the world who are expected to participate in showcasing their collection in Arise Magazine Fashion Week (AMFW) in Lagos, Nigeria to be held from 6th -11th March-2012.
Mustafa Hassanali is the sole Fashion Designer from Tanzania who is expected to participate in this Fashion Week, which continues to acquire popularity in Africa and the world at large, by unveiling his new collection aptly named “Afrikalos”. “The name of my collection Afrikalos is derived from two words, “Afri” shortened version of Africa and “kalos” is Greek word which means beauty. Afrikalos has been inspired by the sight, sounds, rhythm, vibrancy and vivaciousness which truly defined the beauty of our motherland, Africa. The inspiration or chaotic Colour coordination and amalgamation of various textures of fabric and prints, which defines exotic meets eclectic version of innovation that is truly in motion.” Said Mustafa Hassanali. Having shown in 12 Different African countries, and visited over 15, Mustafa Hassanali shall pay a timeless tribute to the nations that have hosted and nurtured his passion for fashion in Africa “I feel so proud and excited to be part of this great African Event for the second time, this shows how our creativity is accepted and growing in every part of Africa. I would like to thank the Arise Magazine team and Mr. Nduka Obaigbena for believing in me. As Mustafa Hassanali brand, this year we have evolved and re-energized our collection with pomp and pageantry”. Concluded Hassanali This year AMFW will be held in the best and popular luxury hotel, Federal Palace Hotel in Lagos Nigeria, from 6th-11th March 2012. This follows those of last year which were witnessed by more than 5,000 visitors, who watched creations from 51 designers. All the best Mustafa ..

Anna Abdalla akerwa na wanaobeza viti maalum

Kuelekea siku ya wanawake duniani
Mwenyekiti wa asasi ya umoja wa wanawake wanasiasa (T-WCP) Mh. Dk Anna Margareth Abdalla, akihutubia katika sherehe za siku ya wanawake zilizofanyika Buza wilayani Temeke, Kulia kwake ni Diwani viti maalum Temeke Mh. Like Gugu na kushoto kwake ni mjumbe wa sekretarieti ya T-WCP na mwisho ni Dk Deus Kibamba kutoka Jukwaa la Katiba Tanzania. MWENYEKITI asasi ya umoja wa wanawake wanasiasa nchini (T-WCP) Mh. Dk. Anna Margareth Abdallah, ameelezea kukerwa kwake na baadhi ya wanasiasa wanaobeza nafasi za viti maalum kwa makusudi na kuzipachika majina yasiyofaa. Mama huyo alitoa dukuduku lake katika sherehe za siku ya mwanamke zilizofanyika katika ukumbi wa Gadafi Buza wilayani Temeke chini ya asasi hiyo ya T-WCP. Kumekuwepo na maneneo maneno juu ya hizi nafasi za upendeleo wanazopewa wanawake na makundi mengine maalum, ambayo kwa kweli ukiyasikiliza wakati mwingine yanakatisha tamaa alisema. “Binafsi naamini kuwa viti maalum ni haki ya mwanamke, hasa ukizingatia namna yeye alivyojitoa kupigania nchi hii kwa kipindi cha zaidi ya miaka 40”. Kwa kipindi chote hicho wanaume wamekuwa mstari wa mbele katika kujpa vyeo na kusahau kabisa nafasi ya mwanamke katika jamii kama hii ya kitanzania. Tatizo pekee ambalo linaweza kuzungumziwa ni utaratibu wa upatikani wa hivyo viti maalum. Lakini kwa kuwa sisi wenyewe tumeshalitambua, tungependa tuachiwe wenyewe. Sisi kama wanawake tutajua jinsi ya kulitatua alisema Mh. Anna Abdalah. Wakati mwingine inakera sana kusikia watu wakiwabeza wabunge wa viti maalum kwa kuwanyima baadhi ya haki ama kuwaita majina yasiyofaa kama vile viti vya chee na Kadhalika hii inakera kwa kweli. “Ushauri wangu kwa wanawake wote nchini watumie nafasi za viti maalum kama shule, kwa kukaa kwa muda mchache na baada ya kubobea kurudi kwa wananchi na kuwapisha wanawake wengina katika nafasi hizo” alisisitiza. “Kwa kuwa utakuwa ushapata uelewa wa kutosha utakaporudi kwa wananchi itakuwa ni rahisi kuingia katika mchakato wa uchaguzi na hivyo kupambana na hatimaye kufanikisha kuchukua nafasi za uongozi”. Mwenyekiti huyo aliwahimiza wanawake kujibidiisha katika shughuli za ujasiriamali ili kujiweka sawa kiuchumi jambo litakalo warahisishia katika kujiunga na michakato mbalimbali hususani ya kugombea nafasi za uongozi. Akitoa mada katika mkutano huo Dk. Deus Kibamba kutoka Jukwaa la katiba Tanzania amewataka wanawake kuelekeza nguvu zao katika kushiriki kwenye mchakato mzima wa uandikwaji wa katiba mpya kwa kutoa maoni yao yatakayofanikishwa kupatikana kwa katiba mpya nchini. “Shuguli ya uandishi wa katiba yetu haiwahusu wanasheria peke yao, hivyo na nyinyi wanawake mnapaswa kuelewa kuwa mna nafasi kubwa ya kushiriki katika uandikishwaji wake kupitia maeneo mbalimbali kama vile tume, bunge maalum na hata kura ya maoni” alisema. Mratibu wa Ulingo wilaya ya Temeke Bi Paskazia Sezari ambaye ndio mwenyeji wa shughuli hiyo aliwataka wanawake kutoa sapoti kwa wanawake wenzao watakaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi. “Msijali ni kwa nafasi gani unachotakiwa kuangalia ni uwezo alionao mwanamke huyo na hivyo kuwajibika kumpigia kura. Hii itasaidi kuongeza kundi la wanawake katika uongozi”. Maadhimisho hayo yaliwakusanya wanawake zaidi ya 300 wa vyama mbalimbali kutoka wilaya ya Temeke wakiwamo viongozi wa ngazi kadhaa yanatarajiwa kufika kilele Machi 8 mwaka huu.
Baadhi ya wanawake kutoka vikundi mbalimbali vya VOCOBA wakisherehekea siku ya wanawake. Sherehe hizo zimefanyika katika ukumbi wa Gadaffi Buza wilayani Temeke jijini Dar es salaam.

Monday, March 5, 2012

Naledi Vintage Catwalk

Ilikuwa ni zaidi ya fashion shoo...hebu cheki
Shukrani sana kwa wabunifu wote pamoja na Kemi Kalikawe mwandaaji ambaye pia ni Founder wa Naledi House of Fashion.

Red Carpet siku ya wanawake - Serena Hotel

Mambo ya wadada na wamama wa mujini, Ilikuwa full Kanga jioneeeeeeee!!!!!!!!!!!!
PICHA ZAIDI TEMBELEA www.8020fashions.blogspot.com

Friday, March 2, 2012

Historia

Matukio muhimu katika siku ya leo


1931: Mikhail Gorbachev aliyekuwa rais wa iliyokuwa Urusi ya zamani azaliwa. Aliongoza taifa hilo tangu mwaka 1985-91

Kiwaloooooooooo

Mapishi


Mahitaji
Margarine, mafuta ya mgando ya nazi ¼ kikombe cha chai
Unga wa kakau (Cocoa Powder) ¼ kikombe cha chai.
Karanga au korosho ¼ kikombe cha chai
Sukari ¼ kikombe
Jinsi ya kutengeneza
Yeyusha mafuta yako hadi yawe ya maji kabisa , weka unga wa kakau, weka sukari koroga hadi vichanganyike, endelea kukoroga ili kuzuia visigande.
Weka karanga au korosho kiasi unachohitaji.

Baada ya hapo imimine kwenye sahani au trei ya bati kisha weka kwenye jokofu kwa muda wa dakika kumi au zaidi.
Ikishapoa itoe katika jokofu na kisha iweke kwenye chombo kwa ajili ya kuikata, hakikisha unatumia karatasi aina ya foil ili kuiweka sawa.tayari kwa kuikata.

Ukishamaliza unatakiwa kuiweka kwenye jokofu kwa ajili ya kuigandisha na kupata ugumu unaohitajika.
Inapendeza kuliwa wakati wa jioni hasa mnapokuwa katika mapunziko ya kawaida.

Naledi..............


BAADA ya kimya cha muda mrefu, Naledi Fashion House kesho itazindua toleo lake jipya kwa mwaka 2012. Shughuli hiyo itafanyika katika hoteli ya Sea Cliff iliyoko jijini Dar es salaam.
Toleo hilo maalum litakusanya mitindo ya aina nne yenye vionjo vya kiafrika vyenye mahadhi ya zamani. Mitindo hiyo ni pamoja na ile ya kiofisi, ya kawaida, ya mitoko ya jioni na hata ile ya sherehe hususani za harusi.
Mkurugenzi wa Naledi Kemi Kalikawe amesema kuwa lengo hasa la onyesho , pamoja na kuonyesha vipaji vya wabunifu chipukizi ni kuwakumbusha wadau kwamba siku zote ya kale ni dhahabu.
“Na hii ndio sababu kubwa ya shoo hii kuitwa vintage catwalj, kwani tutawaonyesha watu mavazi yanayoendana na mandhari ya kisasa ambayo yana vionjo vya kale. Mavazi hayo yamebuniwa kwa ustadi wa hali ya juu hivyo, hakuna shaka juu ya ubora wake” alisema
Katika onyesho hilo kutakuwepo na vionjo mbalimbali vya kale kama vile utengenezaji wa nywele na mapambo mengine.
Baadhi ya wabunifu chipukizi kutoka nchini watakaoonyesha kazi zao ni pamoja na Mgece Mackory, Annette Charles Ngongi, Bambo Fransis Magingo, Garvas Lushaju , pamoja na Ahmed.Pamoja nao kutakuwepo na wabunifu kutoka nje ya nchi ambao ni Palvika kutoka nchini Uingereza.
Pia kutakuwepo na wabunifu watakaoonyesha mapambo kama vile hereni, mikufu na bangili kwa upande wa Tanzania kutakuwako na Mwandale pamoja na Phoeniz Africa. Na pia kutakuwako na Riri kutoka nchini Kenya.
Mbali na mavazi Kemi amebainisha kuwa wanamitindo wote watakaopambwa jukwaani, watapambwa kwa kutumia sanaa ya zamani na hivyo kuzidi kunogesha zaidi shoo hiyo.
Naledi ni miongoni mwa kampuni za kitanzania zinazobuni mavazi kwa kutumia kanga na vitenge, ikiwa na lengo la kuendeleza utamaduni wa mtanzania na mwafrika kwa ujumla.

Thursday, March 1, 2012

Happy birthday Justin Bieber............


Justin Bieber is 18 years old

Justin Bieber was born in 1994

Profession: Musician

About Justin Bieber: Canadian singing sensation first became popular on YouTube

Who am I trivia: My song "Baby" was a worldwide top-ten single