Sunday, June 1, 2008

Mkate wa pasaka



Mkate wa pasaka ni mkate wenye asili ya kigiriki ambapo,kiutamaduni ulibuniwa maalum kwa ajili ya sikukuu ya pasaka.

Mkate huu hunakshiwa na rangi nyekundu ikiwa ni alama ya kuonyesha kumwagika kwa damu ya yesu ikiwa ni moja kati ya imani zao.

mahitaji


Sukari ¼ kikombe Chumvi kijiko 1 cha chaiHamira kijiko kimoja cha chai
Unga wa ngano ½ kiloMargarine 2 vijiko vya chakula.
Maziwa vikombe viwili vya chaiMayai 9 Unga wa ganda la limao vijiko 2 vya chakulaRangi nyekundu kijiko kimoja
Maji kijiko kimoja cha chai

Namna ya kufanya


Hatua ya kwanza


Chukua bakuli la plastiki lenye ukubwa kiasi changanya unga wa ngano,chumvi sukari,hamira na maziwa.
Kanda unga wako hadi ulainike vizuri kisha uweke pembeni.

Hatua ya pili


chukua maziwa vijiko vitatu, changanya na margarine weka jikoni hadi margarine iyeyuke,kisha weka mchanganyiko huo kwenye mashine ya kuchaganyia changanya taratibu,weka na mayai mawili ambapo yai moja litoe kiini na ubakie ute huku ukuendelea kupiga weka unga wa limao.

Hatua ya tatu


Chukua rangi changanya na maji pamoja na unga wa ngano ili upate uji mwekundu.
Chukua mayai mabichi yapake mchanganyiko huo na kuyafanya yaonekane mekundu.

Baada ya hapo chukua unga wako uliokanda na usuke katika umbo la mkufu
Kisha yapachike mayai katikati ya mkufu huo
Chukua chombo cha kuokea paka mafuta na kisha weka unga wako tayari kwa kuoka.

Oka kwa muda wa dakika 30 au hadi uwe na rangi ya hudhurungi,
Chukua mchanganyiko wako namba mbili paka juu ya mkate wako kabla haujapoa.

Mkate wako tayari kwa kuliwa

No comments:

Post a Comment