Chapati ni chakula kinachopikwa na kuliwa sana na watu wa Afrika ya mashariki ,Malaysia na kwa kiasi kikubwa nchini India.
Chapati huliwa kama kitafunwa na waweza kutowelea na mchuzi au mboga au kitoweleo chochote.
Kwa kawaida chapati zipo za aina mbili za maji na za kusukuma.chapati za kusukumwa hupendelewa na watu wengi sana. Lakini je unajua zinavyopikwa kama ulikuwa hufahamu angalia hapa chini
Mahitaji
Unga wa ngano vikombe viwili vya chai.
Chumvi nusu kijiko cha chai
Maji ya moto
Mafuta ya kupikia
Jinsi ya kupika
Changanya unga chumvi na maji. Kanda taratibu hadi uwe umelainika weka mafuta kijiko kimoja endeelea kukanda mpaka uhakikishe mafuta yamekolea kwenye unga.kata matonge manne yaliyo sawa katika umbo la mduara kama chungwa na uache kwa dakika chache.
Chukua donge mojamoja weka paka unga kwa nje halafu weka kwenye kibao cha kusukumia na sukuma hadi iwe katika umbo bapa .paka mafuta sehemu ya juu halafu kunja (roll) baada ya hapo zungusha kupata umbo la mdura ili kurahisisha katika kusukuma .
Sukuma tena kupata umbo la bapa halafu weka chuma cha kukaangia chapati jikono baada ya kupata moto weka chapati jikoni na igeuzegeuze mpaka iive weka mafuta kaanga hadi ikupe rangi ya dhahabu.
Fanya hivyo kwa unga wote ulioandaa .
Andaa chapati zako tayari kwa kuliwa .
No comments:
Post a Comment