Saturday, May 31, 2008

Kaimati

Kaimati ni kitafunwa kinachotengenezwa kwa unga wangano na sukari ambapo sukari hii yaweza kuwa ya shira au ya kukorogea humohumo.

Mahitaji

Unga wa ngano ½ kilo
Sukari ¼ kilo
Mafuta ya kupikia ½ lita
Hamira kijiko cha chai
Unga wa hiliki kijiko cha chai

Namna ya kutengeneza
Chukua bakuli kubwa ya plastiki weka maji vikombe viwili vya chai
Weka hamira
Weka unga wa hiliki
Changanya na upate namna ya uji mzito sana
Uache kwenye joto kwa muda hadi uumuke.

Baada ya kumuka chukua mafuta weka kwenye karai la kukaangia yaweke jikoni hadi yachemke.
Chukua kijiko chota uji wako na weka kwenye mafuta yaliyochemka
Fanya hivyo kwa unga wote

Baada ya kumalizika chukua sufuria nyingine kavu na iweke jikoni
Weka maji kikombe kimojacha chai
Acha yachemke weka sukari ,iache iive na ikishaanza kuwa uji unaonata weka kalimati zako huku ukizigeuzgeuza ilizikolee shira.

Kaimati zako tayari kwa kuliwa waweza kunywa na chai au kinywaji chochote cha baridi.

Mkate wa mayai





Karibu mpenzi msomaji wangu katika safu hii ya mapishi kama ilivyoada kila wiki ninakuletea namna ya kupka aina ya upishi ambao natumai utakupendeza .

Kwa leo nakuletea namna ya kupika mkate wa mayai wa kukunja uluonakshiwa na jam.

Wengi watu tumezoea kula mikate ya kawaida kama vile mkate wa kumimina, mkate wa skonsi na mkate wa boflo lakini mkate wa mayai wa kukunja umekuwa kitu kigeni miongoni mwa watanzania wengi.

Mahitaji
Mayai 6
Sukari vijiko3 vya chakula
Unga wa ngano vijiko 3 vya chakula
Maziwa ya unga vijiko 3
Vanila
Foil
Margarine
Jam
Unga wa soda ½ kijiko cha chai

Namna ya kufanya

Chukua bakuli kavu la plastiki au la kaure
Pasua mayai yote na yamimine katika bakuli weka unga wa soda kisha yapige hadi yatike povu jeupe .
Changanya na sukari huku ukiendelea kukoroga,weak maziwa ,weka unga wa ngano margarine kijiko 1 kikubwa cha chakula,vanilla matone matatu.
Endelea kukoroga hadi upate uji mzito.

Uache mchanganyiko huo kwa muda wa dakika tano huku ukiandaa moto kwa ajili ya kuoka mkate wako .

Andaa trei lenye umbo la pembe nne kwa ajili ya kuoka mkate wako , chukua karatasi la foil na litandaze kwenye trei hiyo.
Mimina mchanganyiko huo na kisha usambaze juu ya foil
Oka kwa moto usio mkali sana .
Baada ya kuiva toa ndani ya jiko na paka jam kwa upande wote wajuu.
Baada ya hapo ikunje (roll) huku ukiondoa foil na kuiacha ilivyo.
Mkate wako tayari kwa kuliwa ,unashauriwa kuweka ndani ya jokofu ili kuufanya upoe na kuleta ladha nzuri zaidi.

Waweza kuliwa na kinywaji chochote cha baridi.

Yai ndani ya fremu/Egg in a Frame


Karibu mpenzi msomaji wa safu hii mapishi, leo nimekuandalia namna ya kuandaa kitindamlo wakati wa asubuhi kwa ajili ya mtoto wako.
Na hii yote ni katika kukurahisishia uandaaji kwani katika kifungua kinywa hiki waweza kutumia dakika tano tu na kupata kile ambacho mtoto wako atakifurahia
Mahitaji
Silesi moja ya mkate.
siagiyai moja chumvi (na pilipili kama utapenda)ili kuongeza ladha.
Namna ya kuandaa.Toa sehemu ya kati ya silesi ya mkate,ipake siagi pande zote mbili kama kawaida na iweke kwenye sahani.
Chukua sehemu ya nje ya mkate ulioitoa ikiwa na umbo kama fremu, na ibandike jikoni kwenye frying pan yenye mafuta, halafu igeuze gauze.
Chukua yai lako na livunje kisha lidondoshee katikati ya ile fremu ya mkate kwenye hiyo frying pan na kaanga taratibu hadi yai live na kuonyesha rangi nyeupe.
Nyunyizia chumvi kidogo na pilipili kama utapendelea, weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa. Hiki ni kitandamlo kwa ajili ya mtoto mmoja

krispy za mbatata



Viazi mbatata ama ulaya kama watu wengi wanavyopendelea kuviita ni kati ya chakula kilicho na mapishi mengi kama vile mchele.

Na mara nyingi vyakula hivyo hutofautina kwa majina kutokana na namna vinavyotengenezwa nah ii ni kutokana na usanii unaofanywa na wapishi katika kukamilisha sanaa hii muhimu.

Krisp ni moja kati ya upishi mmojawapo unaotokana na viazi mbatata, lakini je unajua zinatengenezwaje?

Mahitaji Viazi mbatata kiasi. Chumvi kiasi. Mafuta ya kupikia ya maji. Mashine ya kuparuzia karoti (grating machine) Namna ya kupika Menya viazi vyako , kisha vioshe vizuri.Hakikisha hauuachi na majimaji Unahitaji kuwa na kile kimashine kidogo cha kuparuzia nyanya au karoti(grating machine) au kama huna waweza kutumia kisu kukatakata katika maduara membamba
Vianike kidogo viwe vikavu. weka mafuta, wacha yapate moto. Vimimine ndani ya mafuta, uvikaange
Geuzagauza visishikane. Wacha mpaka viwe rangi ya hudhurungi
Ipua nyunyuzia chumvi , wacha vipoe.Tayari kwa kuliwa

Fagi



Fagi/ Fudge
Hivi unaelewa kuwa vitu vitamu vitamu mfano wa pipi ambavyo mara nyingi huliwa baada ya mlo ‘dersets’ vyaweza kutengenezwa kirahisi?

Kwa kudhihirishia hilo leo tutaangalia namna ya kuandaa na kutengeneza kwa kutumia mahitaji yanayoweza kupatikana jikoni kwako.

Kwa kuanzia waweza kutumia vipimo vifuatavyo na pindi utakapoamua kutengeneza kwa wingi waweza kutumia kiasi unachohitaji kwa uwiano sawa na vipimo hivi.

Haya fuatana nami katika kukupa maelekezo ya namna ya kutengeneza au fagi na kuifanya familia yako ifurahie upishi huu.

Mahitaji
Sukari 1/4 kg
Siagi vijiko 3 vya chakula
Maziwa ¼ kg
tui ¼ kg
Cocoa vijiko 3 vya chakula
karanga ½ kikombe cha chai (zilizosagwa)
chumvi ½ kijiko cha chai
Njia

Koroga cocoa kwa maji.
Injika sufuria tia maziwa, cocoa, tui, na sukari.
Acha mchanganyiko huo uchemke kwa muda wa dakika 30 tia chumvi katika maji ya baridi.
Tia ndani ya sufuria iliyopo jikoni huku ukikoroga ili kuhahakikisha isigande wala kuungua.
Iache ichemke hadi kuwa uji mzito na baada ya hapo ipua na kisha, tia karanga halafu
Chukua bati, waweza hata kutumia sinia la bati, paka siagi kisha mimina uji huo na uache upoe.

Baada ya kupoa katakata vipande fagi zako tayari kwa kuliwa.
Ni chakula kitamu sana kwani ni mfano wa pipi lakini sio pipi halisi hivyo hupendelewa zaidi na watoto na hata wakubwa.

Fagi huliwa kama vile kashata na inapendeza zaidi kama italiwa na kinywaji kisicho na sukari kama vile kahawa.