Saturday, May 31, 2008

Kaimati

Kaimati ni kitafunwa kinachotengenezwa kwa unga wangano na sukari ambapo sukari hii yaweza kuwa ya shira au ya kukorogea humohumo.

Mahitaji

Unga wa ngano ½ kilo
Sukari ¼ kilo
Mafuta ya kupikia ½ lita
Hamira kijiko cha chai
Unga wa hiliki kijiko cha chai

Namna ya kutengeneza
Chukua bakuli kubwa ya plastiki weka maji vikombe viwili vya chai
Weka hamira
Weka unga wa hiliki
Changanya na upate namna ya uji mzito sana
Uache kwenye joto kwa muda hadi uumuke.

Baada ya kumuka chukua mafuta weka kwenye karai la kukaangia yaweke jikoni hadi yachemke.
Chukua kijiko chota uji wako na weka kwenye mafuta yaliyochemka
Fanya hivyo kwa unga wote

Baada ya kumalizika chukua sufuria nyingine kavu na iweke jikoni
Weka maji kikombe kimojacha chai
Acha yachemke weka sukari ,iache iive na ikishaanza kuwa uji unaonata weka kalimati zako huku ukizigeuzgeuza ilizikolee shira.

Kaimati zako tayari kwa kuliwa waweza kunywa na chai au kinywaji chochote cha baridi.

No comments:

Post a Comment