Saturday, May 31, 2008

Fagi



Fagi/ Fudge
Hivi unaelewa kuwa vitu vitamu vitamu mfano wa pipi ambavyo mara nyingi huliwa baada ya mlo ‘dersets’ vyaweza kutengenezwa kirahisi?

Kwa kudhihirishia hilo leo tutaangalia namna ya kuandaa na kutengeneza kwa kutumia mahitaji yanayoweza kupatikana jikoni kwako.

Kwa kuanzia waweza kutumia vipimo vifuatavyo na pindi utakapoamua kutengeneza kwa wingi waweza kutumia kiasi unachohitaji kwa uwiano sawa na vipimo hivi.

Haya fuatana nami katika kukupa maelekezo ya namna ya kutengeneza au fagi na kuifanya familia yako ifurahie upishi huu.

Mahitaji
Sukari 1/4 kg
Siagi vijiko 3 vya chakula
Maziwa ¼ kg
tui ¼ kg
Cocoa vijiko 3 vya chakula
karanga ½ kikombe cha chai (zilizosagwa)
chumvi ½ kijiko cha chai
Njia

Koroga cocoa kwa maji.
Injika sufuria tia maziwa, cocoa, tui, na sukari.
Acha mchanganyiko huo uchemke kwa muda wa dakika 30 tia chumvi katika maji ya baridi.
Tia ndani ya sufuria iliyopo jikoni huku ukikoroga ili kuhahakikisha isigande wala kuungua.
Iache ichemke hadi kuwa uji mzito na baada ya hapo ipua na kisha, tia karanga halafu
Chukua bati, waweza hata kutumia sinia la bati, paka siagi kisha mimina uji huo na uache upoe.

Baada ya kupoa katakata vipande fagi zako tayari kwa kuliwa.
Ni chakula kitamu sana kwani ni mfano wa pipi lakini sio pipi halisi hivyo hupendelewa zaidi na watoto na hata wakubwa.

Fagi huliwa kama vile kashata na inapendeza zaidi kama italiwa na kinywaji kisicho na sukari kama vile kahawa.

No comments:

Post a Comment