Sunday, June 1, 2008

Mishikaki ya nyama ya ngombe

NYAMA ni miongoni mwa vyakula vilivyo na mapishi ya aina nyingi, ambapo mara kwa mara imekuwa ikibadilika majina kutokana na aina ya upishi au namna ilivyo changanywa katika upishi husika.

ifuatayo namna ya kutengeneza mishikaki ya nyamna ya ngombe ikiwa ni moja kati ya aina lukuki za mapishi ya nyama.

Kabla ya kutengeneza mishikaki kwanza kabisa inbakubidi uelewe aina ya nyama ambayo hutumika kutengenezea mishikaki hiyo ili usije jichanganya katika mapsihi yako.

Nyama aina ya “fillet” ndio hasa inayotakiwa katika upishi huu ingawaje wapishi wengi wamekuwa wakitumia nyama yeyote isiyo na mfupa katika kukamilsisha upishi huu.

Mahitaji

Nyama ya ngombe ( filet) 1/2 kilo
Tangawizi iliyotwangwa vijiko 3 vya chakula
Kitunguu saumu kijiko 1 kikubwa cha chakula
Ndimu 1
Chumvi kijiko 1 cha mezani
Masala kiasi (kama utapendelea)
Karoti kiasi
Hoho kiasi
Kitunguu maji kiasi.

Namna ya kutengeneza

Chukua nyama isafishe vizuri kwa maji safi kisha ikatekate vipande vidogovidogo
weka katika sufuria na kisha kamulia ndimu kipande, weka chumvi kiasi, tangawizi na vitunguu saumu vilivyosagwa,
Chukua hoho karoti na vitunguu maji vikatekate kulingana na vipande vya nyama ulivyokata.
Loweka kwa muda wa dakika 15 kisha chomeka katika miti ya kuchomea ukichanganya na viapande vya hoho na karoti bila kusahau vitunguu maji, kisha Andaa jiko la kuchomea na anza kuchoma.
Hakikisha mishikaki imeiva vizuri bila kuungua kwa matokeo mazuri waweza kuichovya kwenye mafuta kidogo ili kuifanya iive haraka.

Baada ya ya dakika 20 mishikaki yako itakuwa tayari kwa kuliwa, waweza kula na chips au hata ugali.

Kababu za mayai



KABABU ni kitafunwa kilichobuniwa kitaalamu zaidi na kukifanya kuonekana cha kuvutia kutokana na umbo na hata ladha yake?

Lakini pamoja na uzuri wake ni watu wachache sana wanafahamu namna ya kutengeneza upishi huu.
Nimeamua kukuletea upishi huu kutokana na maombi ya watu wengi kutaka maelezo ya namna ya kupika kitafunwa hiki.

Fuatana nami upate uhondo huu

mahitaji


Nyama ya kusaga 1/2kg
Mayai 9
kitunguu saumu kiasi
Vitunguu maji kiasi saga
Tangawizi(mbichi) saga
Chumvi kiasi
pilipili manga kiasi
mafuta ya kula lita moja
Mikate wa boflo1
na pilipili kali kiasi kama unatumia.

Namna ya kutengeneza


1) Chukua tangawizi ,kitunguu maji , kitunguu saumu twanga hadi vilainike kisha weka pembeni.
Halafu chukua nyama yako weka chimvi kisha injika jikoni hadi iive halafu ipua.
Chukua mkate wako toa ile nyama ya ndani na kisha uloweke hadi uloanekisha kamua halafu changanya na nyama pamoja na viungo ulivyotwanga kisha weka unga wa pilipili manga huku ukiendelea kuchaganya, ukichanganyika vizuri weka pembeni.
Chukua mayai sita kati ya tisa yachemshe na kisha yamenye halafu weka pembeni.

Chukua mayai matatu yapasue kisha weka chumvi kidogo halafu weka katika bakuli yake.
Tengeneza maduara sita ya kiasi kisha ya huo mchanganyiko kisha weka yai katika kila duara.
Halafu injika jikoni mafuta yakipata moto chovya maduara yako na kisha weka jikoni hadi yawe ya kahawia.Kababu zako

Supu ya uyoga





SUPU ya uyoga ni maarufu sana na inapendwa na watu wengi. Na mara nyingi upikaji wake unatofautiana na kulingana na matakwa ya walaji.

Katika mapishi leo hii nitakuletea namna ya kupika supu ya uyoga na maziwa upishi ambao ni adimu sana kwa walaji walio wengi.

Mahitaji

Uyoga ¼
Unga wa ngano kijiko cha chakula
Margarine (blue band) kijiko cha chakula
Maziwa kikombe kimoja cha chai
Kitunguu saumu viwili vikubwa
Tangawizi mbili kubwa
Chumvi. kiasi

Namna ya kupika

Chukua uyoga wako usafishe na kisha katakata vipande vidogovidogo, halafu kitunguu maji katakata weka kwenye sufuria,chukua tangawizi na kitunguu saumu twanga changanya pamoja, weka chumvi halafu tia lita mbili za maji katika sufuria hilo na kisha chemsha kwa muda wa dakika 20.
Acha ichemke hadi ibakie ujazo wa lita moja au moja na nusu.
Pasha margarine au siagi kaaanga unga wa ngano mkavu hadi ubadilike rangi na kuwa brown, weka maziwa huku ukikoroga.
Endelea kukoroga kwa muda wa dakika 2 hadi 3 kisha weka mchanganyiko uliochemsha awali na endelea kukorga hadi vichanganyike vizuri.
Acha vichemke kwa moto mdogo kwa dakika 5 hadi 10.

Supu yako ipo tayari kwa kuliwa. Na unaweza kuhudumia watu wanne.

Urojo






UROJO ni chakula kilichozoeleka sana Zanzibar,na mara nyingi kimekuwa kikitumiwa sana wakati wa jioni.

Chakula hiki kimekuwa kikiliwa sana hasa wakati wa jioni katika mitaa mbalimbali nchi hasa katika ukanda wa Pwani.

Kutokana na maombi ya wasomaji wengi wakinitaka niwaelezee namna ya kutengeneza upishi huu leo nimeamua kuja nao ili kuwapatia ladha ya kile wanachohitaji.

Urojo hivi karibuni umekuwa ukijulikana kama mix kutokana na mchanganyiko wa vitumbalimbali unaowekwa ili kukmilisha chakula hiki.

Fuatana nami ili ujue namna ya kuandaa chakula hiki chenye ladha ya kipekee

Mahitaji


Mbatata (viazi ulaya) kiasi. Unga wa ngano (1/4 kikombe cha chai) Bizari 1/2 kijiko cha chai (ile ya rangi ya manjano)
Chumvi kiasi. Chatini ya ukwaju
Chatini ya nazi Kababu za kunde au muhogo
Kachori vipande vya figilikrips za muhogo
Namna ya kufanya chukua viazi mbatata osha vizuri weka kwenye sufuria ya maji safi injika jikoni chemsha hadi viive.
Vikishaiva viipue na vitoe kwenye maji kisha vimenye
Vikatekate katika vipande vidogovidogo na weka kwenye bakuli.
Chukua sufuria nyingine weka maji vikombe vinne weka chumvi kijiko kimoja kikubwa
Koroga uji wa unga wa ngano
Hakikisha uji huo unakuwa mwepesi
weka binzari .
Ukishachemka ipua na weka pembeni kwenye bakuli.


Ukishamaliza yote hayo kinachuofuatia ni kuchanganya vitu vyote ulivyonavyo ili kupata urojo halisi.

Chukua bakuli yako yenye ukubwa wa kiasi inapendeza ikiwa ya Kaure.

Weka urojo pawa tatu,kababu za kunde5,kachori 5, kripsi vijiko vitatu vya mezani,viazi mbatata kiasi na mishikaki
Weka chatini ya ukwaju na chatini ya nazi
Halafu katia figili.

Urojo wako tayari kwa kuliwa.

wali wa kichina

mahitaji

Mchele 1 na 1/2 kilo
Kamba wadogo 1kilo (unaweza kutumia kuku aliyechambuliwa au chaza)
Limau/ndimu 1
Carrot 2-3 (osha kata kwa urefu mara 4 ikisha kata slesi)
Njegere 1/2 kilo
Pilipili boga 1(iliyokatwa vipande vidogo)
Yai 1
Viungo kiasi (pilipili manga, uzile, mdalasini, iliki vilivyosagwa)
Vitunguu maji kiasi (kata vya kukaanga na kutwangwa na thomu)
Thomu kiasi (punje 1-2)
Bizari njano kiasi
Mbatata 2-3 (kata ndogo ndogo ukipenda tia)
Maji kiasi
Mayonaise kiasi(ukipenda)
Mafuta kiasi
Chumvi kiasi

Namna ya kupika

Chemsha kitoweo, chumvi, bizari na ndimu hadi kiwive na kiwe kikavu (au na urojo kidogo), chemsha njegere mpaka zisiwive zikawa laini
Twanga thomu, chumvi kidogo, vitunguu maji na viungo vyote
Chemsha wali kwenye maji ya chumvi na uchuje ukiwa una kiini cha kiasi ya kuwiva, weka pembeni
Weka sufuria unayohisi inaweza kuingia vitu vyote, na utie mafuta
Kaanga vitunguu maji kidogo, mbatata, pilipili mboga, carrot na pia vitunguu vilivyotangwa
Unakoroga kwa muda mdogo hadi zionyeshe kuiva, unatia yai na urojo wa kitoweo kidogo (au mayonaise), ikiasha unamimina kitoweo na njegere
Mwisho unamimina wali na unakoroga hadi uchanganyike na halafu unaonja chumvi kwa kulea ikisha unaoka kwa mkaa kiasi ukauke
Baadae unapakua na unaserve kwa saladi