Sunday, June 1, 2008

Mishikaki ya nyama ya ngombe

NYAMA ni miongoni mwa vyakula vilivyo na mapishi ya aina nyingi, ambapo mara kwa mara imekuwa ikibadilika majina kutokana na aina ya upishi au namna ilivyo changanywa katika upishi husika.

ifuatayo namna ya kutengeneza mishikaki ya nyamna ya ngombe ikiwa ni moja kati ya aina lukuki za mapishi ya nyama.

Kabla ya kutengeneza mishikaki kwanza kabisa inbakubidi uelewe aina ya nyama ambayo hutumika kutengenezea mishikaki hiyo ili usije jichanganya katika mapsihi yako.

Nyama aina ya “fillet” ndio hasa inayotakiwa katika upishi huu ingawaje wapishi wengi wamekuwa wakitumia nyama yeyote isiyo na mfupa katika kukamilsisha upishi huu.

Mahitaji

Nyama ya ngombe ( filet) 1/2 kilo
Tangawizi iliyotwangwa vijiko 3 vya chakula
Kitunguu saumu kijiko 1 kikubwa cha chakula
Ndimu 1
Chumvi kijiko 1 cha mezani
Masala kiasi (kama utapendelea)
Karoti kiasi
Hoho kiasi
Kitunguu maji kiasi.

Namna ya kutengeneza

Chukua nyama isafishe vizuri kwa maji safi kisha ikatekate vipande vidogovidogo
weka katika sufuria na kisha kamulia ndimu kipande, weka chumvi kiasi, tangawizi na vitunguu saumu vilivyosagwa,
Chukua hoho karoti na vitunguu maji vikatekate kulingana na vipande vya nyama ulivyokata.
Loweka kwa muda wa dakika 15 kisha chomeka katika miti ya kuchomea ukichanganya na viapande vya hoho na karoti bila kusahau vitunguu maji, kisha Andaa jiko la kuchomea na anza kuchoma.
Hakikisha mishikaki imeiva vizuri bila kuungua kwa matokeo mazuri waweza kuichovya kwenye mafuta kidogo ili kuifanya iive haraka.

Baada ya ya dakika 20 mishikaki yako itakuwa tayari kwa kuliwa, waweza kula na chips au hata ugali.

No comments:

Post a Comment