Sunday, June 1, 2008

Vipopoo

Vipopoo ni upishi ambao unaojulikana sana katika maeneo ya pwani ingawaje mpaka leo haijajulikana asili hasa ya upishi huu.

Naweza kusema haijulikani asili yake kwani upishi huu umekuwa ukipikwa pia na wenyeji wan chi za Japani ,Thailand na maeneo yam engine lakini vikiwa na majina tofauti.

Vipopoo vipo vya aina tatu na vimegawanywa kulingana na aina ya unga unaotumika katika kuvitengeneza.

Waweza kutengeneza vipopoo kwa kutumia unga wa muhogo ,ngano na hata mchele na pamoja na kupisha kutokana na aina ya unga upishi wa vipopoo hivyo ni wa aina moja .

Nasema ni wa aina moja kwani viungo vinavyotumiwa katika upishi huu vinashabihiana kwani kwa kawaida vipopoo huungwa na nazi pamoja na sukari.


Mahitaji

Ungawa mchele 1kg
¼ kijiko cha chai unga wa iliki
tui zito vikombe viwili
½ kikombe cha sukari
maji lita moja
rangi ya chakula


namna ya kutengeneza

weka maji jikoni na yaache ya chemke kama ya ugali na yakishachemka weka unga wa mchele, songa vizuri na mwiko mpaka uwe mgumu kama ugali wa kawaida .
Gawanya katika sehemu mbili au zaidi kutokana na rangi ngapi unatumia.
Ongeza rangi halafu endelea kusonga mpaka uchanganyike vizuri.
Chukua mabonge yako ya unga na yaweke katika ungo wenye unga ili utakapotengeneza visigandane.
Tengeneza vimviringo vidogo vidogo kama vigololi au vyenye ukubwa njugu mawe.
Changanya sukari, kikombe kimoja cha maji, na nazi. Hakikisha sukari imeyayuka kabisa, halafu chemsha.
Weka vimviringo vya mchele kwenye nazi inayochemka, acha vichemke kama dakika tano, ipua.
Weka kwenye vibakuli vya kitindamlo.

No comments:

Post a Comment