Sunday, June 1, 2008

Kamba wa kukaanga




Kamba ni aina ya samaki wanaopatikana kwenye maji chumvi na pia kwenye mito hasa maeneo yenye delta kama vile mto rufiji .

Samaki hawa wapo wa aina nyingi na hutofautiana kwa majina kulingana na ukubwa wake kwani wapo wadogo zaidi hujulikana kama uduvi,wakubwa kidogo wanafahamika kama dagaa kamba na wakubwa wanaitwa kamba kochi.

Lakini kwa leo nitakupa kidogo kuhusiana na namna ya kukaanga kamba na ukapata kitafunwa kizuri kwa ajili ya kinywaji chako.

Mahitaji

Dagaa kamba ½ kilo
Unga wa dengu ¼ kilo
Chumvi
Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa kijiko 1
Mafuta ya kula ½ lita
Ndimu na pilipili kama unatumia
Masala .


Namna ya kufanya


Chukua dagaa kamba wasafishe wakate vichwa na uwamenye maganda yao na kuwaacha nyama ya ndani .
Waweke katika bakuli na kisha changaya na na viungo vyote tangawizi ,vitunguu saumu ,masala ndimu na pilipili chumvi.
Nyunyizia unga wa dengu katika mchanganyiko huo hadi upate uji mzito .

Chukua karai mimina mafuta weka jikoni na baada ya kuchemka kaanga dagaa wako hadi wawe na rangi chungwa .
Fanya hivyo kwa dagaa wote katika bakuli lako na baada ya hapo kamba wako wapo tayari kwa kuliwa waweza kula wenyewe kama kitafunwa au waweza kula kama kitoweo kwa kula na chakula kingine .

No comments:

Post a Comment