My People,Jokate Mwegelo posing with William Malecela at Serena
My People,Jokate Mwegelo posing with William Malecela at Serena
Johnson Lujwangana posing with William Malecela a.k.a Big Show
Ohhh
They love kabelelejr blog
Bro William Malecela posing with Meneja Masoko wa Kampuni ya Kidoti Peter Kasiga
They look poa sanaaaa
Sinta a.k.a JLO wa Bongo,the one and only Christina.Nywele by KIDOTI
We Sinta wewe....Mbona umependeza sanaaaaaaa
OMG......umeuwa wangu,kudadadekiiiiiiiii
Nikaona ngoja nikuvute kama siyo ku-ZOOM huo mkoba,umetokelezea ile mbayaaaa
Mgongo unao,sijabisha hata kidogo mamiiiiiiii
Kumbe hata mguu unalipa...safiiiiiii
Hiyo rangiya kucha tuuuu,maana
Mpaka Big Boss William akaona hapana,ngoja na yeye afanye kweliiiii hahahaha
Nawakubali sanaaaaaaaaaaaaaaaaa
Weraaaaaaaaa,SINTA;SEIF KABELELE;ESI and WILLIAM MALECELA
PARTYY PEOPLEEEEE
Oh yesssssssssssss,Kabelele,Sinta,Esi and MalecelaJr
Dats what am talking about yoooo
BBM ilihusu
Unabisha_
I love them jamani,Bea,Sinta and Jokate
Me love you long time wadada
I love u mingimingi mnoooooooo
Oh Goshhhh
I like dat Jokate
Bro William umetishaaaaaaaaaaaaa
Wen em Tz New Yorkers meet hahahahahaa,Bea and Le Mutuz a.k.a William
Meneja Masoko wa Kampuni ya
Kidoti Peter Kasiga pamoja na CEO wa Kidoti Jokate Mwegelo wakijibu
maswali kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo ambapo pia
amefafanua kuzinduliwa rasmi kwa tovuti ya kampuni hiyo leo
itakayopatikana kupitia anuani ya www.kidotiloving.com
Kidoti ambayo ni chapa halisi ya Kitanzania imezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Chapa ya Kidoti imeundwa katika taswira yake mwenyewe Jokate.
Sifa
zake alizohakikisha zinaonekana kupitia Kidoti ni pamoja na akili,
ujasiri, dhamira, yenye kuthubutu lakini pia yenye bashasha zote za
kike.
Kidoti haitaishia katika mavazi na mitindo tu.
Kidoti ni harakati na mwanzo wa chapa ya mitindo-maisha yenye nia kuu ya kuwezesha kizazi change,” aliongeza Jokate.
Nywele
sanisi za Kidoti ambazo zimezinduliwa leo katika soko ni zenye ubora wa
hali ya juu zikiwa zimejaribiwa na wateja wake watarajiwa wenyewe.
Mtiririko
mzima wa ubunifu na uzalishaji wa bidhaa hizi ulisimamiwa na kuongozwa
na Jokate ambapo kila nywele zimejaribiwa na kukidhi matakwa ya kudumu,
kuweza kutumiwa tena na tena, uzito pamoja na msokotano.
Nywele
hizi zinakuja katika mitindo na urefu mbalimbali ambayo imebeba sifa za
chapa hii zikiwa na mawimbo nyororo kwa ajili ya wanawake wanaopenda
kupendeza bila kufilisi mifuko yao.
Pamoja
na ubora wake wa hali ya juu, nywele hizi zinaendana kabisa na nia ya
Kidoti ya kuvuruga na kuleta maana mpya katika tasnia ya mitindo kwa
ubunifu wa kuweza kutengeneza mitindo mingi kutumia nywele moja na sifa
hii inawasilishwa kwa soko walengwa kibunifu kupitia kasha za bidhaa
hizi ambazo zimesheheni picha za Jokate mwenyewe akionyesha mitindo
mbalimbali kwa ajili ya kila nywele. Sifa hii ya kipekee pia
inawasilishwa kupitia maneno “nywele moja staili kibao!” yaliyochapishwa
katika kila kasha.
Nywele
za Kidoti zitapatikana kwa bei nafuu kupitia mawakala mbalimbali wa
jumla na rejareja jijini kuanzia leo na zitauzwa kwa kati ya Sh. 9,500
na 12,000.
Mawakala
hawa ni pamoja na maduka ya jumla na rejareja Kariakoo, saluni
mbalimbali jijini na mtandao wa mawakala mikoani utakaokuwa na bidhaa
zetu kuanzia wiki ijayo.
Nguo za Kidoti zitatambulishwa rasmi katika soko mwakani (2013) zikifuatiwa na vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi.
Harakati
ya Kidoti inaendeshwa na timu ya vijana wabunifu pamoja na kwamba
shughuli za Kidoti zinaendeshwa kutoka Dar es Salaam, chapa hii ni ya
kiulimwengu zaidi.
Chapa
ya Kidoti ilianzishwa mwaka 2011 na Bi. Jokate Mwegelo ambaye ni mmoja
wa watu mashuhuri nchini, kwa nia ya kubadilisha mtazamo mzima wa tasnia
ya mitindo. Chapa hii itasheheni bidhaa mbalimbali zikiwemo nywele za
sanisi ambazo zimezinduliwa leo pamoja na chapa. Bidhaa nyinginezo ni
pamoja na nguo, vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi.
Kidoti ni chapa yenye uwezo wa kubadilisha jinsi tunavyoichukulia tasnia ya mitindo hivi sasa.Story kwa hisani ya SEIF KABELELE