Wednesday, August 26, 2009

Purple iko 'in' jamani


Hivi unaipenda ' purple' kama ninavyoipenda? ? Je ni kwa vipi unaitumia rangi hii nzuri katika kukamilisha mitindo yako, je unavaa purple katika mitoko yako ya usiku kama ulikuwa hujawahi jaribu uone matokeo yake.

Kwa kifupi ni rangi inayopendwa na watu wengi hasa macelebrities, umewacheki Rihanna na Victoria Beckam Cherlize na christine Aguirela wametoka bomba sio mchezo.

Uzuri wa rangi hii ni kwamba unaweza kuitumia kama ilivyo kwa katika nguo zako au ukiona inakuchanganya pia si vubaya ukatumia accessories zenye rangi hiyo ili kunogesha vazi lako




Tuesday, August 25, 2009

Patchwork accessories ( mapambo ya viraka)































Mtindo wa viraka viraka ni mtindo ambao ulikuwa juu sana katika miaka iliyo pita hasa ya themanini lakini hii leo nimeona bora tumumbushane mana kwa mtazamo wangu naona pia unaweza kupanda muda wowote

Monday, August 24, 2009

Stefanía Fernández miss Universe 2009

Mrembo Stefania Fernández (18) ambaye ni Miss Venezuela amejinyakulia taji la miss Universe kwa mwaka 2009 shindano lililofanyika kisiwa cha Atlantis Paradise kilichopo Nassau, Bahamas.


Nafasi ya pili imeenda kwa Miss Dominican Republic Ada de la Cruz na ya tatu imekamatwa naye Miss Kosovo Marigona Dragusha.

Shindano hilo lilifanyika jana August 23, 2009 ikiwa ni mara ya 58 tangu kuanzishwa kwake, ambapo nchi 84 duniani zilishiriki Tanzania ikiwa mmoja wapo.
Mwakilishi wa Tanzania Illuminata Wize, ameambulia patupu kwani hakuweza hata kuingia kumi na tano bora.

Nchi zilizoingia kumi na tano bora ni pamoja na Albania, Australia, Ubelgiji Croatia, Jamuhuri ya Czech,Jamuhuri ya Dominican, Ufaransa, Iceland, Kosovo, Puerto Rico, Sweden, Switzerland, South Africa, Marekani na Venezuela.

Hii ni mara ya pili mfululizo taji hilo kwenda nchini venezueala ambapo mwaka jana lilichukuliwa na Dayana Mendoza kutoka nchi hiyo

Saturday, August 22, 2009

Miss Universe Africa kesho




Fainali ya kumsaka 'African beauty queen' zinatarajiwa kufanyika kesho, ambapo Tanzania inawakilishwa na mrembo Iluminata Wize,
Warembo wanaoshiriki shindano hilo walipanda jukwaani siku ya jumatatu ya tarehe 10,Agosti 2009 katika ukumbi wa Rainforest Wyndham Hotel ulioko Nassau katika visiwa Bahamas, kwa ajili ya kuonyesha vazi la jioni na vazi la taifa kwa kila mshiriki, ikiwa ni maandalisi ya shindano hilo.

Kesho warembo hao watapanda katika jukwaa la Atlantis, Paradise Island, Bahamas kwa ajili ya kutafuta taji la Miss Universe 2009.

Mungu Ibariki Tanzania, mungu mbariki Illuminata






Mavazi katika mwezi wa Ramadhani








Mfungo wa mwezi wa Ramadhani ni miongoni mwa nguzo tano za uislam, hivyo kama muislamu nimeona si vibaya nikawakumbusha mavazi ya staha yanayopendeza hasa kwa wanawake, haijalishi uwe muislamu ama la.

kwani kujistiri hujenga heshima mwanakwetu, wengi hujiuliza mavazi ya stara ni yapi? lakini wala usikonde hebu cheki hapo juu utafahamu ninachomaanisha.

Cocktail ring nazo zipo juu kwa sasa





Mitindo huenda na kurudi pia ipo ambayo hudumu kwa muda mrefu bila kuondoka. Pete za Cocktail ni miongoni mwa Accessories ambazo zipo juu kwa sasa ingawaje zilishawahi kupendwa katika kipindi cha miaka ya nyuma.
kilichonifurahisha hadi nikaamua kukujuza kuhusiana na mtondo huu, ni ule uwezo wake wa kuvaliwa na watu wa aina mbalimbali na kukubalika hebu jaribu uone

Thursday, August 20, 2009

Butterfly miwani ambayo ipo juu kwa sasa
















Pamoja na kutumiwa kama kinga na tiba ya macho, miwani ni miongoni mwa accessory muhimu sana hasa kwa wale wanaoelewa maana ya mitindo.



wadau wengi hasa mastaa mbalimbali wamekuwa wakitumia miwani kuboresha muonekano wao kama wanavyoonekana hapo juu.



Lakini kwa sasa mtondo wa Butterfly kiasi kwamba wabunifu wengi wamekuwa wakitengeneza aina hiyo

Thursday, August 13, 2009

Aina za viatu kwa kinababa


VIATU ni kati ya mavazi ambayo mara nyingi hayatiliwi maanani sana na wanaume, kama ilivyo kwa wanawake ingawa viatu vya wanaume ni aghali zaidi ya vile vya wanawake lakini je, wanaume hao wanaelewa kuwa uvaaji wa viatu huenda sambamba na mavazi yao na kuchangia waonekane watanashati?

Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wengi hawatilii maanani suala la uvaaji wa viatu katika kukamilisha mavazi yao wengi wao wanadhani wanaweza kuvaa viatu vya aina na rangi yoyote wakatoka bila kujali nguo ulizovaa, shughuli wanayofanya wala hali ya hewa.

Watu wengi wanazingatia kununua tu nguo lakini si viatu. Katika hili wanaume ndio wanaonekana kuathiriwa zaidi na tabia hii, kwani mara nyingi wamekuwa wakionekana kutojali sana mitindo ya viatu.

Suala la kuwa na viatu vingi wao huona kama linamhusu zaidi mwanamke na si mwanaume. Mara nyingi huonekana kutilia mkazo masuala ya utanashati katika kutengeneza ndevu na nywele na nguo na kusahau kabisa kwenda na wakati katika mitindo ya viatu.Tena wapo ambao hawaoni tabu kuvaa viatu vya ofisini nyumbani au katika shughuli ambazo ni tofauti kabisa na mazingira ya ofisi.

Mfano, wanaume ambao ni askari utakuta ni kawaida kwao kuvaa viatu vyao vya ofisini katika sherehe au shughuli nyingine tofauti na zile za kiofisi na kusahau kuwa aina hizo za viatu vinatakiwa kuvaliwa kama sare ya kazini kwenye shughuli za shuluba.

Wataalam wa mambo ya mitindo wanashauri viatu kuvaliwa kulingana na shughuli iliyokusudiwa na wanaume wanatakiwa kuwa na viatu zaidi ya jozi nne, hii itasaidia sana kuwafanya waonekane watanashati na wenye kujua maana katika mitindo na fasheni kwa ujumla.

Kwa vazi la jeans
Suruali ya jeans huvaliwa na viatu vya rangi na aina tofauti tofauti ingawaje wataalamu wa mambo ya mitindo wanashauri kutokuvaa viatu vyenye rangi ya kuwaka sana kwani itapoteza maana.

Buti, raba, makubazi ni baadhi ya viatu vinavyoendana na jeans, hivyo ni jukumu la mvaaji kuoanisha vazi lake na shughuli anayoikusudia kufanya akiwa katika vazi hilo.

Na hakikisha viatu na jeans yako vinaendana na fulana au shati ulilovaa ili usionekane kichekesho katika tasnia ya mitindo.

Kwa nguo za kawaida
Mwanaume kama ilivyo kwa mwanamke huwa anakuwa na shuguli zake za kawaida ambazo si za kiofisi wala sherehe, hapa hulazimika kuvaa mavazi ya kawaida (casual wear).

Katika mavazi haya aina ya viatu inategemea na aina ya vazi hilo kama atakuwa amevaa pensi na fulana au kaptula na fulana unashauriwa kuvaa makubazi au hata raba na utakuwa na muonekano mzuri.

Ikiwa kama una safari fupi na upo katika vazi la pensi ndefu waweza kuvaa buti na ukaeleweka.

Kwa suruali ya kitambaa
Ikiwa utakuwa umevaa suruali ya kitambaa unashauriwa kuvaa viatu vinavyoendana na suruali hiyo mfano unaweza kuvaa kiatu cha ngozi cha kufuta, ili uonekane unayelewa mitindo unatakiwa kuhakikisha kuwa rangi ya viatu vyako inaendana na rangi ya mkanda au ya suruali yako.

Kwa kufanya hivyo utakuwa umeeleweka vizuri katika suala zima la mitindo na pia itakufanya uonekane wa kuvutia na kupendeza.


tips za uvaaji wa viatu kwa wanaume

*Jaribu kuchagua viatu vinavyoendana na suruali yako au vyenye rangi ya giza zaidi ya suruali yako.
*Unapofikiria viatu pia jaribu kufikiria kuhusu soksi hakikisha soksi zako ikiwa umevaa viatu vya kutumbukiza zinaendana na rangi za nguo ulizovaa, mfano haipendezi kuvaa viatu vyeupe na soksi nyekundu.
*Kama umevaa mkanda jitahidi rangi ya mkanda huo ifanane na viatu vyako.

*Hakikisha unakuwa na viatu na mkanda wa rangi nyeusi na vya rangi ya kahawia kwani vitu hivi kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya mitindo vinakubali aina nyingi za nguo. Hivyo inapendeza wanaume kuwa na vitu hivi.

*Ikiwa utavaa kaptula ya jeans au pensi tafadhali hakikisha unavaa na ‘sneakers’ au makubazi na si vinginevyo.

Ni 'blue Iris'


‘Blue iris’ni rangi ya blue iliyokolea na yenye kuwaka, Hii ilikuwa rangi kuu ya dunia kwa mwaka 2008, si hivyo tu kwa mujibu wa wataalamu wa mitindo duniani hii pia imependekezwa kuwa rangi ya msimu kwa sasa ‘colour of season’.

Hivyo basi, kwa kuvaa rangi hii utaonekana ni muelewa wa mitindo na hivyo kuwa wa kisasa zaidi.

Ikiwa una uelewa wa kutosha kuhusiana na suala zima la mitindo nafikiri utakuwa umegundua namna rangi hii ilivyo ‘muhimu’ katika uwanja wa mitindo.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa kipindi hiki kushuhudia warembo wakiwa katika vazi la rangi hii hasa katika mitoko yao ya usiku au shughuli za mchana.

Mavazi ya rangi hii huvaliwa mchana au usiku hii itategemea na namna utakavyolipamba, ikiwa ni maalum kwa usiku yapo mapambo maalum kwa wakati huo vivyo hivyo kwa mchana.

‘Blue iris’inaendana na rangi gani?

Zipo rangi ambazo zikivaliwa na rangi hii huonekana kuvutia zaidi kuliko pale zinapovaliwa peke yake ambapo kwa mujibu wa wataalamu rangi nyeusi na njano na fedha ndio hasa rangi sahihi zinazoendana na rangi hii.

Unaweza kuvaa nguo yanye rangi ya blue na kujipamba kwa kutumia mapambo ya njano, vilevile unaweza kuvaa nguo ya njano na kuinakshi kwa kutumia mapambo blue iris hii ni kwa wakati wa mchana.

Pia si vibaya ikiwa utalipamba vazi hili kwa kutumia rangi ya pink, kwani utaonekana upo juu pia katika mitindo.

Ikiwa utaamua kuvaa vazi la rangi hii kwa wakati wa usiku, italeta maana zaidi ikiwa utaipamba vazi lako kwa rangi ya fedha, kwa kuvaa mapambo yenye rangi hiyo.

Kwa mfano unaweza kuvaa viatu, hereni bangili au kubeba pochi iliyonakshiwa kwa rangi ya fedha hapo utaonekana upo juu zaidi katika mitindo kuliko vile unavyofikiria.

Umuhimu wa rangi ya blue iris katika mitindo.
‘Blue Iris’ ni rangi yenye sifa ya kike, pia inaaminika kuwa endapo itatumika kwa mapambo ndani ya nyumba ina uwezo mkubwa wa kufukuza majini au mapepo katika nyumba na kuiacha huru.

Pamoja na kuvutia kwake rangi hii ina sifa ya kumfanya mvaaji aonekane mwembamba zaidi ya umbo lake halisi. Pia ni rangi ya kujiamini kutokana na uwezo wake wa kuweza kuonekana kwa haraka.

Rangi hii ina sifa zinizofanana na rangi ya njano, hot pink na rangi nyingine zinazofanana hizo, kitendo cha kuonekana haraka kabla ya nyingine hujenga hisia ya kujiamini kwa mvaaji husika.

Unazijua Kashda, au shemagh?




KASHDA ni aina ya kilemba ambacho kiasili kimekuwa kikivaliwa na watu wa nchi za kiarabu,wakijizungushia au kujifunga kichwani na wakati mwingine hadi maeneo ya usoni.
Kilemba hiki wakati mwingine hutumika kama vazi maalum kwa wanaume hasa wanajeshi wa nchi, hasa pale wanapokuwa katika shughuli zao kutokana na hali ya hewa hulazimika kuvaa vazi hili ili kujikinga na jua.
Katika nchi hizo hufahamika kama shemagh au Kefeyah. Hivi sasa kimekuwa katika chati za juu za mitindo kwa kutumiwa kama ‘scarf ‘inayotumika kuzungushiwa shingoni.
Tofauti na ilivyokuwa awali kitambaa hiki kwa sasa huvaliwa na wanawake na wanaume tena wakiwa katika mavazi mbalimbali na kuwafanya waonekane wenye kujua na kujali suala zima la ubunifu katika mitindo.
Katika kipindi cha hivi karibuni kitambaa hiki kimekuwa gumzo kwa wapenzi na wadau wa mitindo, na cha kufurahisha zaidi ni pale baadhi ya wasanii maarufu duniani walipoonekana wakiwa katika vazi hili kitendo kilichochangia kuhamasisha zaidi mtindo wake.
Kanye west mwanamuziki kutoka nchini Marekani ni miongoni mwa wasanii wakubwa walioonekana wakiwa katika vazi hili, ambapo mara baada ya kuonekana mtindo huu ulionekana kupokewa na watu wengi.
Nchini mbunifu wa mitindo Ally Remtullah amekuwa akitumia kitambaa hiki kama pambo lake kubwa ambapo mara kadhaa amekuwa akionekana akijitupia shingini hasa wakati akifanya utambulisho katika maonyesho yake.
Katika mtindo wa kisasa kitambaa hiki huvaliwa kwa kuzingishwa shingoni, au kutupiwa kichwani tofauti lakini huvaliwa katika mavazi tofauti tofauti na watu tofauti tofauti.
Namna ya kuvaa kashda.
Kwa kawaida kitambaa hiki huwa na pembe nne, kikiwa na rangi mboli pia ni huwa ni chepesi na zaidi huwa na urembo kuzunguka pande zote nne.
Kwa kawaida mvaaji hutakiwa kukikunja kitambaa hicho kwa kuchukua pembe moja kuilinganisha na nyingine ili kupata umbo la pembe tatu.
Baada ya hapo unaweza kukivaa katika mitindo mbalimbali kulingana na matakwa yako. Kwani unaweza kukitupia mgongoni huku pembe mbili zikitokea kwa mbele na kukifunga vizuri.
Pia unaweza kujitanda kichwani au wakati mwingine pia si vibaya ikiwa utajizungushia shingoni kwani bado utaonekana unakwenda na wakati.
Mtindo huu kwa kawaida unaendana na mavazi ya aina mbalimbali ingawaje umeonekana kupendeza zaidi katika vazi la jeans, ambapo mvaaji huvaa suruali ya jeans akichanganya na ‘top’ au fulana ya kisasa na hivyo kuonekana bomba zaidi.


Si hivyo tu baadhi ya wadau wa mitindo wamekuwa wakishauri mtindo huu kutokuvaliwa na nguo ndefu sana kwani zinakuwa hazileti maana iliyokusudiwa ambapo mvaaji huonekana kama amebeba mzigo.
Si hivyo tu mtindo huu hutumiwa kama pambo kwa ajili ya kuvaa katika nguo za kawaida (casual) hivyo si sahihi kabisa kuvaliwa katika maeneo ya kazi au kutumiwa na wanafunzi wakati wakiwa mashuleni.
Kwa upande wa viatu unaweza kuvaa na viatu mbalimbali kulingana na aina ya nguo ulizovaa , tofauti na vitambaa vingine kitambaa hiki kinaweza kuvaliwa katika vazi la ufukweni na bado kikaleta maana katika mitindo.

Monday, August 10, 2009

top za silk zipo in mwanakwetu hebu cheki hapa






Wanawake wanene wamekuwa na mahitaji makubwa ya nguo mbalimbali, na mara nyingi wengi wao huamini kwamba ukiwa mwembamba ndio hasa unaweza kupoendeza kwa nguo mbalimbali , lakini si kweli hata kidogo mie napingana nao hebu angalia hapa utakubaliana nami

Blouse kwa waliojazia, upo shost




Unaijua boyfriend jeans? hebu icheki mwanakwetu!


Huu ni mtindo wa uvaaji wa surauali ya jeans ambapo kwa sasa umekuwa katika chati za juu katika mitindo, huko majuu macelebrity kibao wamekuwa wakitoka kihivi